Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na barua kutoka kwa mkuu wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan anayemuomba kumbadilisha mjumbe wake maalumu nchini humo Volker Perthes.
Hii na hatua ya karibuni, katika hatua kadhaa zinazochukuliwa na mkuu huyo wa majeshi, ambaye wiki iliyopita iliyopita alimfuta rasmi wadhifa wa umakamu, mpinzani wake Mohammed Hamdan Dagalo katika baraza tawala
Jenerali Burhan anachukuliwa moja ya viongozi katikati ya mzozo unaoendelea nchini humo kati yake na aliyewahi kuwa msaidizi wake jenerali Mohammed Hamdani Dagalo.
Msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric amesema kiongozi huyo ameshtushwa na ombi la kubadilishwa kwa mjumbe huyo, ambaye kulingana naye anafanya kazi nzuri kama mwakilishi wake.
Perthes na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo wamekuwa wakilengwa na waandamanaji wanaounga mkono jeshi ambao mara kwa mara wamekuwa wakimshutumu kwa uingiliaji wa kigeni na kutaka aondolewe.
Mapigano nchini Sudan yamesababisha vifo vya karibia watu 1,800 kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mashirika ya kufuatilia mizozo.