Waziri wa tamisemi Angela kairuki amepokea na amezingua miradi iliyotekelezwa kwa ufadhili wa shirika la World vision katika wilaya ya korogwe yenye thamani ya bilioni 1.1 inayo husisha sekta ya afya,elimu,nyumba z walimu pamoja na maji ambayo itawanufaisha wananchi zaidi ya Elfu kumi na tatu miasaba.
Waziri amezindua na kupokea miradi hiyo katika ziara yake wilayani humo katika kata za Mnyuzi na kwagunda ambapo amesema kuwa katika sekta ya afya serikali itatoa milioni 150 kwaajili ya kukamilisha zahanati ya Mnyuzi katika Halmashuari ya korogwe vijijini.
“Katika wilaya nzima ya korogwe kwaupande wa watumishi tumesha waletea watumishi wa Afya Harobaini na kama serikali bado tutaendelea kuwalwtea vifaa na vifaa tiba hivyo ndugu zangu watumishi endelee kuongeza kasi ya utoaji wa huduma bora na wananchi wetu waweze kutumia huduma hizo”Alisema Waziri Kairuki
Aidha Waziri Kairuki alisema kuwa kwa wilaya ya korogwe serikali italeta magari ya manne yatakayo hudumia katika sekta ya afya ambapo katika magari hayo magari ma tatu ni magari ya kubebea wagonjwa na gari moja ni kwaajili ya usimamizi wa sekta hiyo.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Idara ya Imani,Maendeleo na Mahusiano ya Umma Shirika la World Vision Dkt.Joseph Mayala amesema kuwa miradi hiyo isinge fanikiwa bila mazingira wezeshi kutoka serikalini kwa ngazi zote,miradi iliyo tekelezwa ni pamoja na vyumba vinane vya madarasa na ofisi ya walimu,madawati miatatu pamoja na nyumba za watumishi,matundu ya vyoo 48 pamoja na ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje pamoja na lengo la kujifungulia na ununuzi wa vifaa tiba.