Sasa ni rasmi Joash Onyango (30) aondoka Simba SC na kujiunga na Singida Fountain Gate FC kwa Mkataba wa Miaka miwili, Singida hawajamtambulisha rasmi wala Simba kumuaga lakini zimevuja picha rasmi akisaini mkataba wa kujiunga na Singida.
Onyango ambaye awali alikuwa anahusishwa na kujiunga na Gor Mahia timu ambayo aliondoka miaka mitatu iliyopita na kujiunga na Simba SC baada ya kuvuja kwa picha hiyo sasa ni rasmi hawezi kurejea tena Singida.
Onyango sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha Singida kinachoelekea Arusha July 10 kwenda kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa 2023/2024.
Kwa stori kamili unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.