Hayo yamesemwa leo tarehe 18/07/2023 wakati wa makabidhiano ya meli ya Mv. Mbeya II kati NIC Insurance na Mamlaka ya bandari (TPA) baada kukamilika kwa matengenezo kufuatia hitilafu ya injini iliyojitokeza kutokana na dhoroba iliyotokea ikiwa inakaribia kutia nanga katika Bandari ndogo ya Itungi (Kiwira) iliyopo Kyela jijini Mbeya.
NIC Insurance imesimamia matengenezo ikiwa ni takwa la kibima kufidia uharibufu uliojitokeza amesema muwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa NIC bwana Hardbert Polepole.
Baada ya matengenezo kukamilika, Meli hii ilifanyiwa ukaguzi na taasisi ya udhibiti wa vyombo vya maji (TASAC) ambapo Meli hiyo ilipewa cheti kwa ajili ya kuendelea kufanya shughuli zake za usafirishaji.
“NIC Insurance imelipa kiasi cha shilingi miliioni 390 kwa mkandarasi Mantrack Tanzania LTD ili kukamilisha matengenezo ya injini na kurejesha safari za Mv. Mbeya II.Tunayofuraha kurejesha huduma za usafiri wa abiria na mizigo ya meli ya Mv. Mbeya II ambayo itaendelea kuchochea shughuli za kiuchumi na jamii kwenye ukanda wa ziwa Nyasa” Ameongeza Polepole.
NIC Insurance inawakikishia wawekezaji wote usalama wa vyombo vyote vya majini.