Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki ufunguzi wa Mkutano wa 18 wa Maspika na Viongozi wa Bunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CSPOC) uliofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Yaounde Jijini Yaounde Nchini Cameroon
Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Cameroon Mhe. Dion Ngute kwa niaba ya Rais wa Nchi hiyo Mhe.Paul Biya leo tarehe 18 Julai, 2023.