Jaguar ni msanii ambae alishiriki kwa kiasi kikubwa sana kwenye kampeni za kumuwezesha Rais Uhuru Kenyatta kuchukua nafasi ya urais wa taifa la Kenya vilevile Jaguar ndio msanii pekee wa kizazi kipya kuingia Ikulu kiurahisi na mara kwa mara kuliko msanii yeyote yule ambapo hii imetokea kwenye utawala wa Rais huyu kijana.
Ukaribu wao umeanzia mbali na ndio maana President hajamsahau Jaguar kwenye ufalme wake ambapo Jaguar kuingia Ikulu ya Kenya sasa hivi sio ishu ngumu kwake na hata anapotaka kuwasiliana na Rais sio ishu yani.
Pamoja na nafasi aliyoipata Jaguar kuwa karibu na Rais na Makamu wake kama inavyoonekana kwenye picha, msanii huyu ameahidi kwamba nafasi hii ataitumia kuwaweka vijana wa Kenya sehemu nzuri kwa kuyawasilisha mapendekezo na matatizo yao moja kwa moja kwenye mazungumzo na Rais.
Rais Uhuru ambae amekua akiendesha mambo kadhaa kiujana zaidi na kuyafanya yawe mepesi kuliko awamu zilizopita, amekua akipokea sifa mbalimbali kutokana na maamuzi yake mengine mfano kutotembea na msafari kila wakati ambapo ili kuepusha gharama lakini pia vilevile usumbufu.
Aliwahi kutembea na gari moja tu Nairobi alafu akasimamishwa na askari wa usalama barabarani ambae baada ya kioo kufunguliwa alishangaa kuona President yuko kwenye hilo gari bila msafara wala kelele za king’ora.
Toka ameingia madarakani, Uhuru amepunguza mshahara wake na wa Makamu wake kwa asilimia 20, Mawaziri pia na viongozi wa mashirika ya Umma walipunguziwa mishahara yao ikiwemo chai na magazeti kufutwa na serikali kwenye bajeti za ofisi zake mbalimbali.
Kama umeipenda hii stori na unataka kila cha millardayo.com kisikupite, unaweza kujiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Instagram facebook ili niwe nakutumia kila kinachonifikia.