Idadi ya wahamiaji wa Sudan wanaokimbia Libya au nchi yao ya asili imeongezeka katika miezi ya hivi karibuni nchini Tunisia. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lilisajili Wasudan 330 huko Sfax mwezi Julai, na kulikuwa na ongezeko la wahamiaji wapya kusini mwa Tunisia katika mwezi huo: watu 860 walijiandikisha, 67% ya watu hao, walikuwa Wasudanhuku wengi wanaishi katika mazingira hatarishi.
Mbele ya ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huko Zarzis, kusini mwa Tunisia, Wasudan zaidi ya mia moja wanasubiri kuitwa kwa nambari zao na majina yao ili kujiandikisha na shirika hilo.
Katika barabara ya kuelekea Medenine, kilomita chache tu, Wasudan wengi wanaishi katika vituo vinavyosimamiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, ambalo haliruhusu upatikanaji wa waandishi wa habari, au hata mitaani, kama Ousmane Ali, ambaye aliwasili Tunisia tangu mwaka 2018.
Mnamo 2019, kadi yake ya usajili ya UNHCR iliisha, na hakuweza kuirejesha. Lakini anataka kubaki nchini Tunisia: “Nimekuwa na matatizo mengi, lakini sijisikii kunyanyaswa au kudhalilishwa hapa. Tatizo ni kwamba kuna kazi ndogo ndogo kwa ajili yetu. Lakini nina marafiki wa Tunisia ambao walinisaidia. ”
chanzo:RFI