Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan mapema leo September 15, 2023 amezindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyopo Mtwara.
Rais Samia amesema kukamilika kwa Hospitali hiyo ambayo ina Wataalamu, vifaa na vifaatiba vya kisasa itasaidia Watu wa Kanda ya Kusini inayojumuisha Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kupata uhakika wa huduma za matibabu ya kibingwa karibu na maeneo yao.
Rais Samia amesema kazi ya Watumishi wa afya ni kuokoa maisha ya Watu hivyo Watumishi hao wajitumie kufanya kazi kwa kuwa Serikali imewekeza kwenye miundombinu, vifaa na dawa na wao watimize wajibu wao “Wagonjwa wote wenye matatizo makubwa watakuja hapa, jengo hili litumike kutoa huduma za afya”
“Tunahitaji matunzo ya jengo hili, vifaa na huduma kwa Wananchi kwa lugha nzuri, kila Mtu amepangiwa jukumu lake na Mwenyezi Mungu, tumridhishe Mungu kwa huduma tunazozitoa, nawatakia kila la kheri, changamoto zilizopo za Watumishi zitaendelea kufanyiwa kazi kwa haraka”