Maafisa wa shirika la hifadhi za Taifa TANAPA,wamepatiwa mafunzo kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Dawati la Ushirikishwaji Jamii ambayo yamelenga kuwajengea uwezo wa namna bora ya ushirikishwaji Jamii.
Akitoa Mafunzo hayo Jijini Arusha katika Ukumbi wa Mikutano wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Mrakibu wa Polisi SP Dkt. Ezekiel Kyogo amesema ulimwengu wa sasa hususani katika masuala ya ulinzi wa rasilimali za taifa unahitaji sana ushirikishwaji wa Jamii ili kuimalisha ulinzi wa rasilimali za taifa.
Ameongeza kuwa maofisa hao wanakila sababu ya kubadilika na kutumia njia ya ushirikishwaji ambayo tafiti zake zimeonyesha kuleta matokeo chanya na ufanisi mkubwa ndani ya Nchini hata mataifa yaliyoendelea kiteknolojia.
Dr Kyogo amesema wataendelea kutoa mafunzo ili kuboresha utendaji kazi wa maofisa hao wa shirika la hifadhi za Taifa TANAPA mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,TAWA na TFS.
Pia akitoa shukrani kwa niaba ya kamishna wa Polisi Jamii CP Faustine Shilogile amesema Kamisheni hiyo inaushukuru uongozi wa wizara ya maliasili na utalii chini ya Waziri Mheshimiwa Angellah Kairuki na makatibu wake kwa kuwapa fulsa ya kutoa mafunzo ya namna bora ya kushirikisha wananchi katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu hususani ule unaofanyika katika mbuga za wananyama zilizopo hapa Nchini.