Michuano ya kombe la dunia imeendelea tena jana usiku kwenye mechi nne kuchezwa.
England ilikipiga na Italy kwenye mchezo ulioanza saa saba ya usiku kwa saa za Afrika mashariki.
Matokeo ya mchezo huo yalikuwa ushindi wa 2-1 kwa Italy, Mario Balotelli akiibuka shujaa kwa goli la ushindi.
Marchisio alianza kuipatia goli la kuongoza Italy kwenye dakika ya 35, kabla ya Sturridge kusawazisha dakika 2 baadae na mchezo kwenda mapumziko sare.
Kipindi cha pili Super Mario Balotelli akaifungia Italy goli la ushindi.
Mchezo mwingine kwenye kundi hilo linalohusisha timu za Costa Rica na Uruguay ulichezwa majira ya saa 4 usiku.
Uruguay wakiwa bila staa wao Luis Suarez wakafungwa 3-1 na Costa Rica.