Madereva waliohitimu mafunzo ya udereva wa magari makubwa katika shule ya udereva kilwa road VTC Academy driving School iliyopo katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam DPA wameaswa kuwa mabalozi kwa madereva na watumaiji wengine wa Barabara ili kupunguza ajali zinazosababishwa na baadhi ya madereva wazembe hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo Novemba 08,2023 na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam DPA kamishna msaidizi mwandmizi wa Polisi SACP Dkt Lazaro Mambosasa wakati akitoa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya udereva wa magari makubwa yaliyofanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja chuoni hapo.
Dkt ameongeza kuwa chuo hicho ni miongoni mwa vyuo vikongwe hapa nchini ambapo amewaomba maderva hao waonyeshe utofauti wa umahiri wao na maderva wanaosoma vyuo vingine huku akibainisha kuwa tayari serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imeendelea kuboresha bandari hapa nchini ambapo amewambia wategemee kuwepo kwa magari makubwa ambayo wataendeshwa na maderva hao walio nasifa na vigezo.
Kwa upande wake afisa mnadhimu namba moja wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam DPA Kamshna msaidizi wa Polisi ACP Obadia Nselu amesema dereva mzuri na mahiri ni yule anayefuata sheria za usalama barabarani huku akiwaomba madereva hao waliohitimu mafunzo ya udereva katika shule ya Kilwa road VTC Academy driving School kuwa mfano mzuri wa kuigwa hapa nchini.
Nae Mratibu wa mafunzo ya udereva katika shule ya Udereva kilwa Road VTC Academy driving School mrakibu msadizi wa Polisi ASP Martine Nyangindu amebainisha kuwa wanafunzi hao wamefundishwa mbinu mbalimbali za kuepuka ajali ikiwemo udereva kujihami ili kujilinda na kuwalinda watumiaji wengine wa Barabara.
Upendo Nnko muhitimu wa mafunzo ya uderva wa magari makubwa ameushukuru uongozi wa shule ya udereva kwa namna ambavyo wamefundishwa na kuwajengea uwezo mkubwa katika udereva wa magari makubwa huku akibainisha kuwa watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa madereva wasiofuata sheria za usalama Barabarani.