Kesi dhidi ya Esther Lungu, aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu, imeanza mjini Lusaka.
Esther Lungu ameshtakiwa kwa wizi wa magari matatu, wizi wa hatimiliki ya mali huko Lusaka pamoja na kupatikana na $400,000 (£317,000) zinazodaiwa kupatikana kwa njia za kihalifu.
Aidha ameshtakiwa pamoja na maafisa wawili wa polisi.
Mmoja wa mashahidi aliiambia mahakama siku ya Jumatatu kwamba Esther Lungu alichukua kwa nguvu gari lake na hati miliki ya nyumba yake pamoja na magari mawili ya bintiye.
Aliongeza kuwa maafisa wa polisi walioshtakiwa waliwalazimisha kutia saini hati za mali hizo kwa mke wa Lungu.
Washtakiwa walikanusha makosa hayo walipokamatwa kwa madai ya mwezi Septemba.