Afisa wa polisi aliyemuua George Floyd amedungwa kisu na mfungwa mwingine katika gereza moja katika jimbo la Arizona kusini magharibi mwa Marekani.
Shambulio hilo limetokea katika Taasisi ya Shirikisho ya Kurekebisha Tabia, Tucson, gereza lenye ulinzi wa kati ambalo limekuwa likikumbwa na utovu wa usalama na uhaba wa wafanyakazi.
Ofisi ya Magereza imethibitisha kuwa mfungwa mmoja alivamiwa huko FCI Tucson mwendo wa 12:30 ioni Ijumaa ya jana.
Mfungwa huyu ambaye awali jina lake halijatajwa, alifikishwa hospitalini baada ya kupatiwa huduma ya kwanza. Maelezo ya hali ya afya ya Derek Chauvin hayajatolewa.
Derek Chauvin, aliyekuwa afisa wa polisi wa Minneapolis, ambaye ndiye aliyemuua Mmarekani mwuesi, George Floyd, anatumikia kifungo baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mauaji kwa sababu za kibaguzi.
Chauvin, 47, alipelekwa FCI Tucson kutoka gereza la jimbo la Minnesota lenye ulinzi mkali zaidi mnamo Agosti 2022 ili kutumikia kifungo cha miaka 21 kwa kukiuka haki za kiraia za George Floyd na kifungo cha miaka 22 na nusu kwa mauaji ya daraja la pili.
Floyd, ambaye alikuwa Mmarekani mweusi, aliuawa mnamo Mei 25, 2020, baada ya Chauvin, polisi mzungu, kumkandamiza goti shingoni kwa dakika 9½ barabarani nje ya duka la bidhaa.