Ni longtime kidogo ulikua hujamsikia Nakaaya na hii ni kwa sababu alikua na break ya uzazi akiwa ndio amejifungua mtoto wake wa kwanza nyumbani kwao Arusha.
Mwimbaji huyu ambae ujazo wa jina lake uliongezeka baada ya kutoa ile single ya ‘Mr. Politician’ sasa hivi anamiliki mawimbi na single yake mpya inaitwa ‘blessing’ aliyoifanya Noizmekah Arusha.
Nakaaya ameamua kuifanya hii single mpya kama dedication kwa mtoto huyu aitwae Kai kuonyesha ni jinsi gani amemgusa moyoni, vilevile kumpa ahadi ambayo ni mama pekee anaiweza.
Bonyeza hapa ili kuisikiliza na kudownload bure mtu wangu >> SIKILIZA HAPA
Ukishadownload na kuusikiliza kupitia MKITO usiache kuniandikia comment umeuonaje ili Nakaaya akipita hapa jioni aone ulichomuandikia mtu wangu.