Manchester United na Borussia Dortmund wamehitimisha mkataba wa Jadon Sancho kujiunga na klabu hiyo ya Bundesliga kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. Kifurushi hicho kina thamani ya €4m (£3.4m) kwa United kulingana na ada ya mkopo na malipo ya sehemu ya mshahara wa winga huyo.
Sancho atapima afya kabla ya kusaini Dortmund, ambao hawana chaguo la kumnunua. Sancho aliimarika katika klabu ya Dortmund kuanzia 2017-2021, jambo lililoifanya United kulipa pauni milioni 73 kwa ajili yake, lakini muda wake Old Trafford umegeuka kuwa mbaya na hajacheza kwa zaidi ya miezi minne.
Sancho ameondolewa kwenye kikosi cha kwanza baada ya kukataa kuomba msamaha kwa Erik ten Hag kwa kumuita meneja huyo muongo.
Sancho alipoachwa nje kwa kipigo cha 3-1 dhidi ya Arsenal, Ten Hag alisema ni kwa sababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alikuwa hajafikia viwango vinavyohitajika mazoezini. Muda mfupi baadaye, Sancho alichapisha kwenye mitandao ya kijamii kwamba maelezo hayo “hayana ukweli kabisa”.