Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa , Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amesema kuna haja ya Viongozi kuwa wakali katika kujenga Chama Cha Mapinduzi kuliko mtu binafsi kwakuwa lengo ni kujenga kwa maslahi mapana ya Chama Cha Mapinduzi na Taifa kwa ujumla.
” *Kuna haja ya kuwa wakali kujenga chama chetu ba sio mtu binafsi, kuna watu wanakuwa wakubwa kuliko chama na watu na kupelekea baadhi ya watu wanaowasujudia kusahau kama chama ndio kimewapa heshima waliyonayo na badala yake kudhira kupiga kura au kutoka hadharani kukisema chama chake na kukataa msimamo wa chama chake* ” Alisema Mwenezi Makonda.
Pia, Mwenezi Makonda Asisitiza ni muhimu kusimamia hilo na kuwaambia Viongozi wa chama kuwa wao ndio kiungo na msingi wa mafanikio ya Chama Cha Mapinduzi.
Aidha, Asisitiza juu ya kuongeza idadi ya wanachama na wenye kadi za uanachama na kulipia ada lakini pamoja na kadi ya mpiga kura kwani ndio tiketi pekee ya kumfanya mtanzania kupiga kura katika chaguzi zote kuanzia za serikali ya mtaa mwaka huu wa 2024 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Hayo yamejiri wakati Mwenezi Makonda akizungumza na Wajumbe wa Kamati za Siasa za Mkoa wa Pwani na Wilaya zake zote alipowasili kwa ziara ya siku moja mkoani humo leo tarehe 19 Januari, 2024.