Msanii wa muziki wa BongoFleva amefunguka baada ya watanzania kumshambulia juu ya jitiada zake ambazo amekua akizionesha kwenye kuwahi kuandika nyimbo za misiba ya viongozi mbali mbali wanao kuwa wametangulia mbele za haki.
Peter amesema kuwa yeye halipwi wala hanufaiki na kuandika nyimbo za misiba wala kuperform Kwenye shughuli za misiba kama watanzania wanavyomuandamana sana sana kuna Muda anatumia gharama zake kufanikisha ambayo amekua akifanya
Hayo yamekuja baada ya muda mfupi kupita Rais Samia kutangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya Pili Hussein Mwinyi ndipo watanzania wakaanza kumtania msanii Peter Msechu kupitia mtandao wa Insta na Wtsap wakidai ataingia studio kufanya wimbo kitu ambacho alifanya hivyo
Msechu amefunguka hayo leo hii akiwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaama wakati wa kuaga mwili wa Hayati Mwinyi ambaye anatarijia atazikwa kesho Unguja