Kamishna wa Polisi Zanzibar C.P Hamad Khamis Hamad amewataka viongozi wa Chama cha act wazalendo na chama kwa ujumla kuacha tabia za kutoa taarifa za kuzua taharuki na kwamba pindi wanapotaka ufafanuzi wafike kwenye mamlaka za polisi.
Cp Hamad ameyasema hayo akidai uwepo wa taarifa zinazosambzwa na chama hicho maara kwa maara kwa kulikosoa Jeshi hilo kwenye utendaji kazi na kudaiwa kutoa matamko ya kupotosha na kutoa maelekezo kwa kuwataka wawakamate wahusika kwenye matukio ambayo jeshi hilo tayari hua limeshachukua hatua jambo ambalo hamad amelitafasiri kama kujinufaisha kisiasa
“Ni kutafuta kujinufaisha kisiasa matukio mengi wanayotoa matamko inawezekana ni kweli ama madai tu ,wanawahusisha wale ambao ni Victim na chama chao cha Act wazalendo ,katika tamko lao la hivi karibuni walisema uwepo wa vikundi vya uhalifu kila siku bila ya Jeshi la Polisi kuonyesha Uwezo wa kudhibiti kwa kukinga ama kufanya upelelezi unaopelekea wahusika kutiwa hatiani ,ni uthibitisho wa utamaduni unaoendelea wa baadhi ya viongozi wa Act kutothamini juhudi za serikali na tasisi zake –CP Hamad