Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuhakikisha changamoto zote
za wafanyakazi inazitatua kwa wakati, ikiwemo kutoa posho la nauli a 50, 000 kwa
wafanyakazi watakaostahili, kutoa huduma bora kwa wananchi na kuendelea kukuza
uchumi wa nchi
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi duniani, (Mei mosi) Uwanja wa Gombani, Wilaya ya Chakechake Mkoa
wa Kusini Pemba
Aidha Rais Dk. Mwinyi ameiagiza Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na
Uwekezaji, kukutana mara nne kwa mwaka na vyama vya wafanyakazi wakiwemo
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar (ZATUC) ili kutatua kwa haraka
changamoto za wafanyakazi badala ya kusubiria Kila mwaka
Rais Dk. Mwinyi alieleza kuwa Serikali itazidi kuhakikisha mazingira ya kazi pamoja
na maslahi ya wafanyakazi yanaimarika ili kuongeza ufanisi kazini.
Alisema ndani ya kipindi cha miaka mitano Serikali imejipangia kutengeneza ajira
300,000 kwa wananchi wake kwa mujibu wa llani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025
Nakuongeza ndani ya kipindi cha miaka mitatu, Serikali kupitia shughuli mbalimbali
za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, Skuli, vituo vya
afya na hospitali, bandari, miundombinu ya maji, umeme na shughuli nyenginezo
imepelekea kupatikana kwa ajira mpya 187,651sawa na asilimia 104 ya lengo la ajira
180,000 kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita,
Akizungumzia posho ya Shilingi 50,000 Rais Dk. Mwinyi alisema Serikali itatoa fedha
hizo kwaajili ya nauli za kwenda kazini na kurudi nyumbani kwa watumishi wote
wanaostahiki kulipwa posho hilo.
Alisema, jumla ya Shilingi 34,099,500,000 zimetengwa na Serikali kwa ajili ya posho
la usafiri. Aidha, alisema Serikali imedhamiria kuhakikisha inaongeza fedha kwa ajili
ya posho ya likizo ambapo jumla ya TZS. 2,523,814,700 zimetengwa na Serikali kwa
ajili ya likizo katika bajeti mpya ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei mosi yenye kauli mbiu kuimarika
kwa maslahi na Mazingira ya kazi ni msingi wa ufanisi kazini* kwa Tanzania bara
yameadhimishwa Arusha