Dubai imetangaza ujenzi wa msikiti wa kwanza duniani unaoelea chini ya maji wenye thamani ya dola milioni 14.9.
Nusu moja ya muundo itakuwa juu ya maji pamoja na maeneo yake ya kukaa na duka la kahawa, ambapo, nyingine imezama chini, kulingana na picha za dhana zilizoshirikiwa na Khaleej Times.
Na upande wa chini ya maji kitakachotumika kama eneo la kuombea, muundo wa kwanza kama huu ulimwenguni utakuwa na sakafu tatu.
sehemu ya kipekee ya kutoa maombi chini ya maji utabeba waabudu wapatao 50-75.
Vyumba vya kuogea na bafu pia vitakuwepo na zaidi ya hayo, wanaoabudu watakuwa na uzoefu wa kipekee wa kutoa sala zao chini ya maji.
Huku Idara ya Masuala ya Kiislamu na Shughuli za Usaidizi (IACAD) mjini Dubai ikifanya kikao fupi kuhusu mradi wake wa utalii wa kidini, mipango kuhusu msikiti huo ilitangazwa.