Mkali huyo wa R&B alipokea tuzo hiyo kutoka kwa Kenneth “Babyface” Edmonds, L.A. Reid, Jimmy Jam, na Terry Lewis Jumapili, Juni 30, katika Usiku Mkubwa wa Cultures, huku mkewe Jenn Goicoechea Raymond akimshangilia kwa furaha na bashasha.
Wakati wa hotuba yake ya , alitafakari juu ya maisha yake kukua bila baba yake na kufuatia hayo, aliamua kuidedicate tuzo hiyo kwa wanaume wote .
“Sitaki kuchukua muda mwingi, lakini nataka kusema kitu, ni muhimu kuelewa kuwa baba ni muhimu sana,” mwigizaji huyo aliyeshinda Grammy aliendelea baada ya dakika 10.
Alihitimisha hotuba yake kwa kusema kila kitu kilihusu kulea watoto wake na umuhimu wa baba wa sasa, akitangaza 2024 kuwa “mwaka wa baba.”
“Kwa akina baba wote usiku wa leo nyumbani au katika hadhira hii, ningependa ninyi nyote msimame kwa sekunde mbili tu kwa ajili yangu” na kusisitiza umuhimu wa kuwatambua baba kama wanavyofanya kwa akina mama mara nyingi.
“Hatuna nafasi ya kusema vya kutosha,kusifu Baba, kwa hivyo hii ni ya wanaume wote huko nje kuwa majenerali kwa wana wao na motisha kwa viongozi wetu weusi wa baadaye,” Usher aliongeza.
“Vijana, asanteni sana kwa heshima hii.”