Najua kuna stori nyingine huwa zinaandikwa alafu wahusika wakuu wanakuja kuziongelea baadae kwa kushangaa kilichoandikwa ambacho mara nyingi kinakua sio cha kweli.
Stori ya Wema kutopatana na ‘mama mkwe’ yaani Mama mzazi wa Diamond ni miongoni mwa stori ambazo kuna uwezekano umeshawahi kukutana nazo kwenye Magazeti au baadhi ya mitandao, stori ambazo zilianza kuandikwa tu baada ya mastaa hawa kurudi mapenzini.
Sasa kwenye exclusive na millardayo.com Wema anasema ‘Watu wanasikia vitu vingi hata kwenye Magazeti watu wanaandika vitu vingi hususani Waandishi huwa wanatengeneza ili tu kupata habari lakini hatuwezi kusema kila kitu kinachotuhusu sisi kila mtu anajua….. hapana, mbona mimi na mama tunapatana tuuuu’
‘Mbona mami ake wangu mieeeee…. mwenyewe ananiitaga chizi langu, kwa hiyo tuko okey sana, nadhani watu wanamawazo hayo kwa sababu Mama ni mama yake Naseeb na mwisho wa siku Naseeb anakua sometimes hivi sometimes vile yeye kama mama lazima asimame nyuma ya mtoto wake ila mama yuko okey, mama ni mchizi wetu.. kamanda wetu mwenyewe’
Ungana na mimi kwenye twitter instagram na facebook niwe nakutumia kila kinachonifikia iwe usiku au mchana mtu wangu, bonyeza hapa >>> INSTA TWITTER FB
Unaweza kumsikiliza Wema akiongea hapa chini.