Taylor Swift amempa onyo Kijana anayefuatilia safari za ndege yake ya kibinafsi kwa kutumia mitandao ya kijamii ambapo timu ya kisheria ya Taylor ikiongizwa na Wakili wake, Katie Wright Morrone, kupitia Barua ya kisheria walimtaka Jack Sweeney kuacha tabia hiyo wanayosema kuwa inahatarisha usalama wa msanii huyo.
kijana huyo alifahamika kwa jina la Sweeney ambaye anamiliki akaunti inayofuatilia ndege hiyo ya Taylor, hali ambayo imesababisha hofu kubwa kuhusu usalama wake, na Mawakili wa Taylor walisema kwamba watachukua hatua za kisheria endapo Sweeney hatasitisha tabia yake.
Katika majibu yake, Jack Sweeney alikiri kwamba hakuwa na nia mbaya, akisisitiza kwamba amefajya hivyo kwa ajili ya uwazi na habari kwa umma, pia alisema kuwa kuguatiliwa kwa safari za ndege ni jambo la kawaida, na aliongeza kuwa huenda hii ikawa sababu ya malalamiko ya umma kuhusu matumizi ya ndege ya Taylor na athari zake katika mazingira.
Kabla ya kufuatilia safari za Taylor Swift, Sweeney anaripotiwa kuwa alifanya hivyo pia kwa mkurugenzi mtendaji wa Tesla, Elon Musk, lakini alikabiliwa na adhabu kwenye mtandao wa X baada ya Musk kumtuhumu kwa kufanya uhalifu.