Sean “Diddy” Combs amewashutumu maafisa wa serikali na waendesha mashtaka kwa kuvujisha taarifa kinyume cha sheria kuhusu kesi yake.
Inaripotiwa kuwa Wanasheria wa Combs wamelalamikia uchunguzi wa idara ya usalama wa ndani kuhusu upekuzi wa nyumba zake na waendesha mashtaka waliotoa video ya mwaka 2016 ikimuonyesha Combs akimshambulia mpenzi wake wa wakati huo, Casandra Ventura. Video hiyo, ambayo ilichukuliwa na CNN, ilitumiwa na waendesha mashtaka kama ushahidi, wakidai kwamba Combs alijaribu kumhonga mfanyakazi wa hoteli aliyeingilia kati wakati wa tukio hilo. Combs alikiri kuhusu video hiyo na kuomba msamaha.
Kupitia jalada la mahakama, Combs, ambaye anshikiliwa bila dhamana, ameeleza kuwa uvujishaji wa taarifa hizo umesababisha maoni mabaya ya awali ambayo yanaweza kuharibu mchakato wa kuchagua majaji na kumnyima haki ya kusikilizwa kwa haki.
Aidha, Wanasheria wa Combs wameomba kusikilizwa kwa ushahidi na kuchunguzwa zaidi kwa ushahidi uliotolewa, wakati huo huo, Combs ameomba kesi yake ianze mapema msimu wa masika wa mwaka 2025, akidai haki yake ya kusikilizwa haraka japo kuwa waendesha mashtaka hawajatoa msimamo kuhusu tarehe ya kesi lakini wamesema wapo tayari kufuata ratiba ya Mahakama.
Combs, ambaye amekana mashtaka dhidi yake, anaendelea kuzuiliwa bila dhamana huku akisubiri kesi yake lakini pia anakabiliwa na mashitaka mengine ya madai kutoka kwa wahasiriwa kadhaa, ambapo amekanusha pia mashitaka hayo ya jinai.