Shirika la Usalama wa Afya la Uingereza limetangaza siku ya Jumatano Oktoba 30 kwamba limegundua kisa cha kwanza cha maambukizo ya aina mpya ya virusi vya Mpox, ambavyo chimbuko lake kubwa ni kutoka barani Afrika.
“Shirika la Usalama la Afya la Uingereza (UKHSA) limegundua kisa kimoja cha binadamu kilichothibitishwa cha clade 1b Mpox,” shirika hilo limendika katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, likibainisha kuwa “hatari kwa raia bado ni ndogo”.
Shirika hilo limebaini kwamba “kisa kimoja cha binadamu kilichothibitishwa cha clade 1b mpox” kimegunduliwa London na kinamhusu mtu “ambaye alikuwa amesafiri hivi majuzi katika nchi za Afrika” zilizoathiriwa na lahaja hii.
Mamlaka za afya zinabainisha katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba “hatari kwa raia bado ni ndogo”.
Mgonjwa aliyeambukizwa lahaja hii mpya aligunduliwa nchini Ujerumani zaidi ya wiki moja iliyopita. Wagonjwa wengine waliripotiwa nchini Sweden na nchi kadhaa za Asia.
“Watu wote waliotangamana na mgonjwa huyu watatakiwa kufanya vipimo na chanjo ikiwa ni lazima na watashauriwa juu ya huduma ya ziada inayotolewa ikiwa wana dalili au ikiwa vipimo vitaonyesha dadili yoyote ya ugonjwa huo,” llimeongeza shirika la usalama, British Health Authority ( UKHSA).