Hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Kagame Cup imeanza leo kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo Azam FC kukupiga na El Merreikh ya Sudan.
Kwenye mchezo huyo kipa kinda wa miaka 19 wa Uganda, amedaka penalti ya Lionel Saint- Preux na kuipeleka El Merreikh ya Sudan Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuitoa Azam FC ya Dar es Salaam.
Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda- Azam walikosa penalti mbili, nyingine Shomary Kapombe aliyegongesha besela na kutoka nje, wakati Merreikh walikosa moja, ya Nahodha Elbasha Ahmed iliyookolewa na kipa Mwadini Ali.
Penalti za Azam zilifungwa na Aggrey Morris, Didier Kavumbangu na Erasro Nyoni, wakati za Merreikh zilifungwa na Alan Wanga, Magdi Abdelatif, Ayman Said na Ali Gefer.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa wa Kenya, Andrew Otieno, dakika 90 zilimalizika kwa sare ya 0-0, ngome za timu zote zikiwa imara haswa.