Job Ndugai ni Naibu spika wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania lakini pia ni mjumbe kwenye bunge la katiba na pia mwenyekiti wa kamati namba 8 kwenye bunge la katiba.
September 12 2014 aliwasha kipaza sauti bungeni na kusema > ‘Nimesimama hapa, nitakayoyasema ni yangu mwenyewe na sio yale ya kamati’
- Ingekua ni vema kama mchakato huu wa katiba mpya ungemalizika katika kipindi hikihiki ambacho Rais Kikwete ni Rais, sababu yeye ndio muasisi wa jambo hili…. wako wanaoshangilia kwamba iende 2016, unampangiaje Rais ajaye vigezo vya vipaumbele vyake? ukishaanza kuweka viraka kwenye katiba ya mwaka 1977 sasa una haja gani ya katiba mpya?
-
Kwenye chama cha mapinduzi tumeahidi kwamba tuaendelea na serikali mbili zilizoboreshwa, kwenye zilizoboreshwa hapa mapendekezo yangu ni kwamba Mabunge yabakie mawili, baraza la Wawakilishi na bunge la Jamuhuri lakini bunge la Jamuhuri liwe na ajenda mbili za kudumu, mambo ya muungano na yasiyokuwa ya muungano.
3. Yamekuwepo malalamiko ya Zanzibar kuhusu mafuta na gesi kwamba itoke katika orodha, kwa sababu wenzetu ni Wadau mi nafikiri jambo hilo liwe hivyo japo ukiniuliza mimi ningependa libaki.
- Kuhusu utawala, Mh. Rais amepewa madaraka na mamlaka kadhaa ya kuwa na uteuzi mbalimbali wa kufanya, ushauri wangu ni kwamba pale alipopewa nafasi ya uteuzi vilevile apewe nafasi ya kutengua uteuzi wake, kwanini nasema hivyo? wako watu walioteuliwa na Mh. Rais lakini ndio wanaopita huko kumpinga kila kukicha.
Kuhusu Mawaziri wakuu… mimi siwasemehi wala sijaongea nao lakini watu waliopita kwenye nafasi hiyo hapa bungeni nimeona wamekua wakitokwa jasho sana, iko haja ya kuangalia namna ya kuimarisha ofisi ya Waziri mkuu… kwa yeyote anaeweza kuwa Waziri mkuu, kumpa madaraka zaidi Waziri mkuu ya utawala na utendaji, kwa mawazo yangu…. ifike mahali Waziri mkuu aweze kuajiri wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya ikiwezekana hata Mawaziri.
Tunavyosema Waziri mkuu ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni kwa kweli awe na madaraka makubwa zaidi ya kuweza kuwasimamia hawa, awe na uwezo mkubwa zaidi kuliko uwezo ambao tumempa Waziri mkuu wa leo.
Kama ni kiu yako stori yoyote inayonifikia isikupite, ungana na mimi kwa kuwa mwanafamilia mtu wangu…. bonyeza hapa >>> Insta twitter Facebook