Siku saba baada ya kutoshana nguvu na viongozi wa ligi Chelsea, vijana wa Manuel Pellegrini Manchester City leo walisafiri mpaka KC Stadium kucheza dhidi ya Hull City.
Iliwachukua dakika saba tu Manchester City kuandika goli la kwanza kupitia Sergio kun Aguero na muda mfupi baadae Edin Dzeko akaifungia City goli la pili kwa mkwaju mkali nje ya eneo la 18 la Hull City.
Vijana wa Steve Bruce wakapambana na kufanikiwa kupata goli la kwanza baada ya Eliaquim Mangala kujifunga wakati akizuia krosi ya hatari golini kwake dakika ya 21, na dakika 11 baadae Hull wakapata penati ambayo iliwekwa kimiani na Hernandez.
Mpaka mapumziko timu zilikuwa zimetoshana nguvu.
Kipindi cha pili magoli mawili ya Frank Lampard na Edin Dzeko kwa mara nyingine tena yakawapa ushindi wa 4-2 dhidi ya Hull City.
Timu zilipangwa
Hull City: McGregor 5.5; Rosenior 6.5, Dawson 6.5, Davies 6, Robertson 5.5 (Brady 83); Elmohamady 6, Diame 6.5, Huddlestone 6, Livermore 5.5 (Ben Arfa 74, 6); Hernandez 6.5 (Ramirez 74, 6), Jelavic 7
Substitutes not used: Bruce, Chester, Harper, Quinn
Scorers: Mangala own goal 21; Hernandez pen 32
Manchester City: Caballero 5, Zabaleta 6.5, Mangala 4.5, Clichy 5.5, Kompany 6.5, Silva 7 (Demichelis 76, 6), Fernandinho 6 (Jesus Navas 66, 6), Yaya Toure 6.5, Milner 6, Aguero 6.5 (Lampard 71, 7), Dzeko 8
Substitutes not used: Hart, Sagna, Kolarov, Pozo
Scorers: Aguero 7; Dzeko 11, 68; Lampard 87
Booked: Mangala, Clichy
Referee: Anthony Taylor 6
Star man: Sergio Aguero