NIPASHE
Mwanafunzi wa shule ya msingi Dar mwenye miaka saba ameuawa kikatili baada ya kubakwa,kuchinjwa kisha kunyofolewa sehemu za siri.
Mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alifanyiwa kitendo hicho kisha mwili wake kutupwa katika shamba la jirani na nyumbani kwao maeneo ya Mbezi Temboni.
Mama wa mtoto huyo alisema mara baada ya mwanaye kurejea akitokea shule alimwogesha kisha kumpa chakula kabla ya kumwacha kidogo na kutoka huku mtoto huyo akienda kucheza na wenzake na aliporudi hakumkuta.
Anasema baada ya kumtafuta bila mafanikio yoyote kwa siku nzima kesho yake walisikia mwili wake umeokotwa kwenye shamba la jirani na mtu mmoja anashikiliwa na polisi kuhusiana na tuhuma hizo.
NIPASHE
Hospitali za Serikali hapa nchini zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa damu baada ya Mpango wa Damu Salama NBTS kukosa baadhi ya vifaa vya kupimia damu kuhakikisha ni salama kwa matumizi.
Meneja wa maabara Hospitali ya Mwananyamala Julius Kisinga alisema hospitali hiyo ina upungufu mkubwa wa damu ukilinganisha na mahitaji ya wagonjwa.
Alisema matumizi ya hospitali kwa siku ni uniti15 hadi 20 kwa wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu lakini kwa sasa wanapata uniti4 hadi 7.
Uchunguzi wa NIPASHE ulifanywa katika hospitali mbalimbali na kugundua tatizo hilo lipo kila mahali na huenda ikatishia maisha ya wagonjwa wenye kuhitaji damu.
MWANANCHI
Hofu imewagubika wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule ya Msingi Mji mpya iliyopo Wilayani Temeke baada ya kuwepo kwa taarifa za kubomolewa shule kupisha ujenzi wa majengo ya biashara.
Taarifa za kubomolewa kwa shule yenye wanafunzi zaidi ya 2,000 zilianza kusambaa baada ya kubomolewa nyumba zote zinazoizunguka shule hiyo.
Mmoja wa wazazi wenye wanafunzi shuleni hapo alisema kamati ya maendeleo ya kata imeshaanza taratibu za kutekeleza ujenzi huo wa majengo ya biashara unaosimamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Temeke.
MWANANCHI
Mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Kabwe Mkoani Rukwa anashikiliwa na polisi kwa tuhumza za kuvamia walimu wa shule hiyo akiwa na silaha aina ya gobore na kufanya uporaji wa fedha na simu nne.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kutoka Wilayani humo zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku ambapo mwanafunzi huyo alivamia nyumbani hapo na kuwakuta walimu hao wakila chakula cha usiku ndipo alipowaamuru kutoa fedha kwani tayari wamelipwa mishahara hivyo lazima wagawane.
Baada ya kuona hali inakua mbaya walimu hao walilazimika kutoa sh75,000 walizokua nazo pamoja na simu ndipo mwanafunzi huyo akaondoka nazo.
MWANANCHI
Kijana mmoja nchini Kenya alilazimishwa kutembezwa akiwa mtupu mtaani ili kuchangisha fedha za kumuwezesha kufanyiwa tohara.
Hatua hiyo ilikuja baada ya kijana huyo kudai hana pesa ya kwenda kufanya tohara na wanaume wenzake kuamua kumtembeza mitaani ili aweze kusaidiawa kupatiwa kiasi cha pesa kitakachomwezesha kufanyiwa huduma hiyo.
Kiongozi wa kundi lililokua likimtembeza mitaani Peter Mwogera alisema lengo la kumzungusha mitaani uchi ni kutaka jamii ya watu wa Githurai waamini kuwa kijana huyo alikua hajafanyiwa tohara.
MZALENDO
Wamiliki wa kampuni 11 kati ya19 zilizofungiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma PPRA kushiriki kazi za umma kutokana na udanganyifu na kushindwa kutekeleza masharti ya mkataba wamebainika.
PPRA ilitangaza mapema wiki hii kuzifungia kampuni hizo kuomba kushiriki zabuni za umma kutokana na kushindwa kutimiza masharti.
Kufungiwa kwa kampuni hizo zikiwemo zinazomilikiwa na wafanyabiashara wakubwa nchini kunatokana na PPRA kufanya ukaguzi kwenye taasisi za Serikali .
MZALENDO
Baadhi ya wananchi Mkoani Simiyu hukataa misaada inayotolewa na wahisani kwa madai ya kutolewa na freemason ambapo huhofia kupoteza maisha.
Diwani wa kata ya Mwabuzo Chalya Seni alisema kuna baadhi ya viongozi wanapotosha wananchi kuwa misaada inayotolewa ni ya freemason na kujenga hofu kwa wahitaji kugoma kupokea.
Aliwatahadharisha viongozi wa kisiasa kutotumia mpango huo kuomba kura kwa wananchi kwa kuwa unaangalia kaya zote zenye uhitaji mkubwa wa misaada na pia hukwamisha jitihada za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi wake.
MZALENDO
Kijana David Matijala raia wa Afrika kusini amekua akiishi na mtu aliyefariki kwa zaidi ya miaka 20 sasa.
Matijala alisema juzi kuwa mtu huyo ambaye ni ndugu yake alifariki zaidi ya miaka20 iliyopita na huwa anajisikia furaha kumuona kila wakati kwani amekua akishiriki nae mambo mbalimbali kama kuongea na kupanga mikakati mbalimbali ya maisha wakiwa pamoja kana kwamba yupo hai.
Kijana huyo alisema anakusudia kwenda kanisani ili nyumba yake iombewe kwa sababu wamekua wakiiogopa na kwamba hata watoto aliozaa na mke aliemkimbia wamegoma kurejea nyumbani kwake.
Inasemekana matukio ya watu kuishi na mizimu nchini Afrika Kusini ni ya kawaida lakini katika miaka ya hivi karibuni yamekua yakihusishwa na imani za kishirikina pamoja na imani za utajiri.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook