Bomu lililotengenezwa kienyeji huko Cairo, Misri limelipuka karibu na mahakama kuu siku ya Jumanne tarehe 14 mwaka huu na kujeruhi watu 12 ambapo gari na maduka yaliliyokuwa karibu ya eneo hilo la tukio yameharibika.
Haikufahamika vizuri kama lengo lilikuwa ni la kumuua mtu mmoja au kufanya tu uharibifu kwa sababu hii ni mara ya pili tukio kama hili limetokea huko Cairo chini ya mwezi mmoja.
Ripoti zinasema bomu ambalo lililipuka mwezi uliopita karibu na wizara ya mambo ya nje lililoua polisi watatu, lilisababisha uhalifu mkubwa ambao haukutokea kwa muda mrefu mjini Cairo.
Shambulizi hilo la bomu lilianzishwa na kundi la Jeshi la Kiislamu liitwalo Ajnad Misr ambapo inasemekana ongezeko la mashambulizi ya majeshi ya Kiislamu yamezidi kwenye nchi hiyo toka mkuu wa jeshi aitwae Abdel Fattah al-Sisi ampindue Rais Mohamed Morsi mwaka jana baada ya wananchi kupinga utawala wake.
Baada ya kumpindua Rais Mohamed Morsi mkuu huyo wa jeshi Abdel Fattah alivunja udugu wa Kiislamu uliokuwa chini ya Mohamed Morsi ambapo serikali ililitangaza kuwa ni kundi la kigaidi.