Siku moja baada ya kampuni ya Apple kufanya uzinduzi wa simu za iPhone 6 na iPhone 6+ nchini China, mapya yameibuka katika mitandao kuhusiana simu hizo.
Kuingia kwa simu hizo katika soko la China, kumezalisha stori mbali mbali ikiwamo hii niliyokutana nayo leo katika mitandao, nikaona ni vyema ‘kushare’ na wewe mtu wangu wa nguvu, na hii ni kuhusiana na kile ambacho watumiaji wa simu hizo wamekiita ‘tatizo la kipekee’.
Tatizo linalozungumziwa na wateja hao kuhusiana na simu hizo ni suala la ukubwa wa simu hizo kupelekea kushindikana kuingia na kutosha katika mifuko ya kawaida ya nguo ambayo tumezoea kuweka simu zetu.
Kutokana na ‘tatizo hilo’, fundi mmoja wa kushona nguo kusini magharibi mwa jiji la Chongqing, aliamua kuitumia fursa hiyo kwa kufungua ofisi ya kushonesha mifuko ya suruali za jeans ambayo ingeweza kutosheleza aina ya simu hiyo kukaa vizuri.
Fundi huyo amesifiwa kuwa mbunifu wa hali ya juu, ambapo amefungua ofisi hiyo ndogo nje ya duka linalouza simu hizo, akiwa na mashine ya kushonea ambayo ni ya muundo wa kizamani, huku akiwa amening’iniza bango linalotangaza huduma yake ya kipekee.
Picha zilizowekwa mitandaoni zikimwonesha fundi huyo zimepata “likes” chache kutoka kwa wapenzi wa Apple nchini China.
Mbali na baadhi ya wateja kulalamikia ukubwa wa simu hizo, bado wapo watumiaji wa simu hizo waliotoa pongezi kwa kusifia ubunifu uliofanywa katika simu hizo ikiwa ni pamoja na maboresho ya ukubwa wa kioo ambao unawapa urahisi wa namna ya kuandika, kuperuzi na pia kutazama video na movie.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook