Masaa machache baada ya kutokea tukio la shambulizi la risasi katika bunge la Canada lililopelekea mwanajeshi mmoja na askari wa bunge, kuuawa serikali ya Canada imetoa tamko rasmi kuhusiana na tukio hilo.
Akitoa tamko hilo waziri mkuu wa Canada Stephen Harper amesema shambulio hilo ‘haliitetemeshi’ Canada, bali linaiongezea nchi hiyo ujasiri.
Rais wa Marekani Barack Obama na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron wamelaani kitendo hicho kwa kukiita ni cha kukiita ni cha ‘kikatili’, huku wakisisitiza kuwa wakati huu ni wa kuwa macho zaidi kwa kuimarisha ushirikiano baina yao katika kupambana na ugaidi.
Cameron ameeleza kuwa tayari kushirikiana na Canada kwa msaada wowote utakaohitajika katika kukabiliana na hali hiyo.
Taarifa kutoka shirika la utangazaji nchini Ufaransa RFI linasema bado askari polisi wa kikosi maalum cha usalama wameendelea kulizunguka eneo hilo japo hali ya usalama imeimarika kwa sasa.
Askari wa bunge Kevin Vicker aliyemuua kwa kumpiga risasi mshambuliaji aliyevamia jengo hilo amepongezwa kwa kitendo chake cha kijasiri na kujitolea.
Canada imesema mwanajeshi aliyeuawa katika shambulio hilo koplo Nathan Cirillo amekufa kishujaa, huku polisi wakiendelea kumsaka mshukiwa wa tukio hilo aliyetajwa kwa jina la Michael Zehalf- Bibeau.