Rapa kutoka La familia Ilala Chid Benz mchana wa October 28 amesimamishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Mashtaka matatu yanayomkabili Chid Benz ni;-
- Kukutwa na madawa na vifaa vya kutayarishaji uvutaji wa madawa
- Kusafirisha madawa ya kulevya
- Utumiaji wa madawa ya kulevya
Kwa sasa Chidi Benz amerudishwa rumande hadi Novemba11 ambapo kesi yake itatajwa tena, kuhusu dhamana ya mshtakiwa mahakama imesema itakuwa wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika na jumla ya pesa taslim million 1.