Rapper Rashid Abdallah Makwiro aka Chid Benz ambaye yupo nje kwa dhamana kufuatia kukamatwa na dawa za kulevya uwanja wa ndege Dar es salaam leo Nov 11 2014 alikwenda tena kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam.
Taarifa kutoka mahakamani kwenye upande wa Jamhuri zinasema upande huo umeomba kesi ya msanii huyo ipelekwe mpaka December 1 2014 mpaka upelelezi ukamilike.
November 10 2014 Chidi Benz aliandika kwenye page yake ya twitter >>> ‘Kesho napanda mahakamani asubuhi pale kwa hakimu mkasi Kisutu, niombeeni kheri koz najua wapo wanaohitaji bado. #vitu mbalimbali‘
Wakati mkali Chidi Benz akiwa kwenye matatizo haya, single yake iliyomrudisha kwenye airtime kwa nguvu kubwa kutokana na ukali wake ft. Diamond na Ay inazidi kuchukua nafasi yake kwenye mikono mbalimbali ya MaDJ.
https://www.youtube.com/watch?v=qJLyuE5Od2M