Familia ya THT imemuachia rasmi msanii Amini Jumatatu ya November 10 ambapo alifanyiwa sherehe rasmi ya kuagwa na kukabidhiwa kwenye kamouni mpya ambayo imeanza kufanya nae kazi.
BME ndiyo kampuni mpya ambayo imemchukua Amini na ndiyo imeanza kufanya nae kazi,ambapo Mkurugenzi wa kampuni hiyo amesema wameamua kuanza na zaidi ya Milion 40 za Kitanzania kwa ajili ya Amini kwa kazi zake za mwanzo.
Amini ameachia wimbo wake wa kwanza unaoitwa Mbeleko akiwa na kampuni hiyo kutoka BME Amini anakuwa msanii wa kwanza kujiunga na kampuni hiyo.
source:255 Clouds FM.