Kwenye hii picha ya kwanza inaonekana sehemu ya kupaki pikipiki aina ya Bajaji ambapo kibao chake kimezibwa kuzuia bajaji zisiingie ndani, kwenye siku ya kwanza bajaji zilikuwa zinaingia ndani na kulipa sh.500 kila wakitoka na abiria ila ilipofika mida ya mchana walikatazwa kuingia ndani.
Kwa taarifa zilizotoka kwa uongozi wa kituo hicho siku kadhaa zilizopita ni kwamba wanapanga utaratibu maalumu na watazisajili bajaji 20 tu ambazo zitaruhusiwa kuingia ndani.
Ni kituo kipya cha Mabasi ambacho kimechukua nafasi ya kile kidogo cha Ubungo kilichokuwepo karibu na TANESCO, hiki kipya kilichopo Sinza kilianza kufanya kazi October 23 2014.