UHURU
Polisi kituo cha Bwaloni,Mbezi kwa Msuguri Jijini Dar wameingia matatani baada ya kudaiwa kusababisha kifo cha mtoto mchanga wa umri wa miezi sita,aliyekua akishikiliwa na mama yake mzazi kwenye chumba cha mahabusu cha kituo hicho.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kituo hicho zinasema baada ya polisi hao kubaini kuwa mtoto huyo amefariki dunia waliamua kumuachia mama huyo na maiti ya mtoto huyo kisha kutokomea kusikojulikana.
Baba mkubwa wa marehemu Shedrack Mwangu alisema polisi hao walifika nyumbani kwa mdogo wake majira ya saa2 usiku na kumkamata shemeji yake kwa madai ya kugombana na jirani yake.
Alisema hatua hiyo inatokana na shemeji yake huyo kumdai jirani yake fedha za upatu anayejulikana kwa jina la Mama Na ambaye alikua akimsumbua na kumdanganya wanachama wenzake bado hawajawasilisha.
Alisema shemeji yake alinyimwa dhamana na ndipo baba wa mtoto alipowaomba askari hao kumchukua mtoto kutokana na hali yake kudhorota ili wakampe dawa lakini walimkatalia na ilipofika alfajiri wakamtaka mama huyo kuondoka kwa madai wao wanakwenda katika kazi zao huku tayari mtoto huyo akiwa amefariki dunia.
UHURU
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amesema kwa sasa hana ushirikiano wowote na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na amejikita zaidi katika kazi zake za Bunge na kwamba suala la upatanishi kati yao ili kuimarisha chama hicho ni uvumi.
Alisema taarifa hizo amekua akizisikia kama wanavyosikia wananchi wengine na kwamba hakuna mzee yoyote Kigoma aliyempa taarifa rasmi na hakuna ushirikiano wowote kati yake na Mbowe.
Zitto alisema hawezi kuzungumza lolote kuhusu msimamo wake kutokana na suala la kutokuwepo na ushirikiano kati yake na Mbowe,kwani kufanya hivyo ni kutoa maamuzi yake kwa jambo ambalo hana taarifa kamili.
“Ninaendelea na kazi zangu za Bunge na sina ushirikiano wowote na Mbowe,hivyo siwei kuzungumza maamuzi yangu kwa taarifa za juu ju,nasubiri kama Taarifa hizo zipo Wazee wangu wa Kigoma watanieleza,hapo sasa nitafunguka”alisema Zitto.
Zitto alitoa ufafanuzi huo baada ya taarifa kuenea kuwa Mbowe alikwenda Kigoma kukutana na wazee wa Kimila na kuunda kamati kwa ajili ya upatanishi kati yako.
MWANANCHI
Serikali imesema itatumia askari wa kimataifa wa Interpol kukabiliana na utoroshaji madini ya vito ya Tanzanite nje ya nchi.
Hatua hiyo inakuja huku Kenya na India zikiongoza kwa kuuza Tanzanite kwenye soko la dunia mwaka jana na kuizidi Tanzania ambako ndiko madini hayo hupatikana pekee duniani.
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri wa madini Richard Kasesela alisema Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kuchunguza na kubaini njia na mbinu zote zinazotumika kutorosha madini hayo nje ya nchi.
“Kuanzia sasa yoyote atakayekutwa akiuza madini nje ya nchi bila cheti cha uhalisia kinachothibitishwa yametoka Tanzania kupitia njia halali,atakamatwa na kurejeshwa nchini na kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi,”alisema Kasesela.
Alisema Serikali haiwezi kuendelea kuvumilia madini na rasilimali zinazopatikana nchini kuendelea kunufaisha watu wa Mataifa mengine.
MWANANCHI
Matukio ya wizi wa watoto Mkoani Kilimanjaro yameongezeka kutoka watoto wanne mwaka 2013 hadi watoto 127 mwaka huu,hali ambayo imezua hofu kwa wazazi na wakazi na Mkoa huo.
Mratibi wa kupingana na ukatili wa kijinsia kanda ya Kaskazini Hilary Tesha alisema takwimu hizo ni kuanzia January hadi Novembermwaka huu
Tesha alisema wizi wa watoto umekua ukihusishwa na imani za kishirikina na sasa unaonekana kuanza kuota mizizi.
Alisema imefika wakati kwa jamii kutoa taarifa mara wanapoona ama kugundua mtandao unaohusika na utekaji watoto na mbali na hilo pia matukio ya ubakaji yameongezeka kutoka matukio 24 hadi31 kwa mwaka.
Alisema chanzo cha matukio hayo yanasababishnwa na matumizi ya dawa za kulevya ndani ya jamii zinazotuzunguka na kuongezaka unywaji pombe kiholela.
MWANANCHI
Utafiti uliochapishwa na jarida la Microbiome la Uingereza limeonyesha kuwa upigaji busu unaweza kusafirisha zaidi ya bakteria milioni80 kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Daktari Sophianis Nyomyani wa Hospitali ya Mwananyamala anazungumzia utafiti huo na kusema bakteria wengi ambao huambukizwa kwa njia ya busu na wengi huchukulia busu kama njia pekee ya kuonyesha upendo.
Utafiti huo pia umesema wapenzi ambao hupigana mabusu kwa wastani wa mara tisa kwa siku huwa na bakteria ambao wanaendana na hubadilishana kila wanapofanya tendo hilo.
“Ni upendo ila kiafya si salama,hata kama wanandoa wanashiriki katika kupigana busu,isiwe kwa kila mtu,ni lazima kuwe na mipaka,unaweza kumbusu mtu shavuni,nje ya mdomo,mkononi na kwingineko lakini siyo lazima mdomoni.
HABARILEO
Kituo cha afya Nguruka Mkoani Kigoma kinakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi hali iliyofanya mlinzi wa usiku katika kituo hicho,BoazSelelo kutumika kama mtoa huduma katika kliniki ya baba,mamana mtoto.
Hali hiyo inatokana na ongezeko kubwa la akinamama wajawazito waliohudhuria kliniki sambamba na kuwahi kituo cha afya wakati wa kujifungua ikiwa ni matokeo ya kampeniinayojulikana kama Thamini uhai,okoa maisha ya mama na mtoto inayoendeshwa na shirika la World Lung Foundation.
Akizungumzia hali hiyo mlinzi huyo alisema baada ya kumaliza zamu yake ya ulinzi usiku analazimika kusaidia kufanya kazi kwenye kwenye kliniki ya wazazi kutokana na kutukuwepo na wahudumu wa kutosha kuhudumia wajawazito hao.
Kwa upande wa mmoja wa wauguzi wa Zahanati hiyo alisema ongezeko la kina mama wajawazito limewalazimu kufanya kazi kwa saa24 ili kuokoa maisha ya wanawake hao pamoja na wagonjwa wengine huku akiiomba Wizara husika kuangalia jinsi ya kuongeza wauguzi hasa katika hospitali zilizopo maeneo ya vijijini.
Mganga mkuu Albert Mumwi amekiri kuwepo na tatizo la upungufu wa wauguzi na wamekua wakipata wagonjwa wengi ambao huzidi uwezo wa idadi ya wataalam wa afya waliopo katika hospitali hiyo.
HABARILEO
Vita ya kusaka urais nchini Zimbabwe imeingia katika hatua nyingine baada ya ndugu watatu wa familia ya aliyekua Rais wa nchi hiyo Michael Sata akiwemo mjane wake Christine Kaseba kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mdogo kupitia chama tawala.
Mjane huyo ameungana na mtoto wa kiume wa Marehemu Sata aitwaye Mulenga Sata mwenye miaka47 ambaye pia ni meya wa jiji la Lusaka na binamu yake Milen Sampa mwenye miaka44 ambao wote wamethibitisha kuwania nafasi hiyo ya juu katika uchaguzi utakaofanyika Januari2o mwakani.
Mjane huyo alisema bado anaomboleza kifo cha mumewe ambaye alizikwa wiki iliyopita na kwamba kitendo cha kuona kazi alizoanzisha mumewe hazikukamilika,zinaiumiza nafsi yake hivyo kuamua kuwania urais ili aziendeleze.
“Maumizu ninayoyapata yatakua ya bure ikiwa sitatimiza ndoto za Rais Sata alizopanga kufanya akiwa madarakani”Mjane huyo alikaririwa na kituo kimoja cha redio nchini humo.
HABARILEO
Serikali imekopa kiasi cha shilingi bilioni50 katika benki ya CRDB kwa ajili ya kununulia mahindi yaliyojazana kwa wakulima nchini,kutokana na kupata mavuno mengi mwaka huu.
Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema fedha zitawawezesha Wakala wa Taifa NFRA kununua mahindi hayo ambayo wakulima wamekosa soko la kuyapeleka kwa sasa.
Aidha amewaagiza wakuu wa Mikoa nchini kuruhusu wakulima kuuzamazao yao katika nchi zenye mahitaji ya chakula hicho kama vile Sudan,Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Alikiri kuwa kutokana na mpango wa kilimo kwanza,Tanzania imezalisha mahindi mengi ambayo yanailisha sehemu ya Afrika Mashariki na pia kuilisha Afrika ambapo mwaka jana kulikua na zaidi ya tani 300,000 za mahindi lakini mwaka huu kuna zaidi ya tani milioni1.5 wakati ziada ya mpunga ni zaidi ya tani800,000.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook