Diamond ndio ameshatoboa mpaka kwenye headlines za muziki wa Nigeria baada ya kushirikiana na wakali wa muziki kutoka kwenye nchi hiyo kama Davido na Iyanya ambapo sasa ni zamu yake na mwimbaji Waje ambae ndio kamshirikisha.
Wimbo huu alioshirikishwa Diamond unaitwa ‘coco baby’ ambapo kwa asilimia kubwa video hii imepata comments nyingi kutoka upande wa Afrika Mashariki pia baada ya watu kujua ni Diamond kapewa shavu.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook