Heard ya leo Desemba 10 inamhusu msanii ambaye alikuwa Kigoma kwenye show na akaazima hela akiahidi kwamba ataituma akifika Dar lakini baadaye hakumtumia mtu aliyemuazima pesa hiyo na alipompigia simu alipokea akamjibu kwamba yuko location ana shoot video.
Baada ya Soudy Brown kumtafuta msanii huyo Linex, amesema kwamba ni kweli aliazimwa pesa na jamaa huyo lakini toka amefika alikuwa anaumwa hivyo akashindwa kutuma hela hiyo lakini leo ndiyo siku aliyopanga kumtumia hiyo na sio kweli kwamba amepanga kumdhulumu.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook