Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Diamond Platnumz:Nimesikitishwa Sana na habari zilizoandikwa na moja ya chombo cha habari, kuwa eti nliwanyanyasa wasanii wenzangu Nyota ndogo na Susumila, kwa kuwafukuza kwenye VIP lounge na sijui eti niliwazuia wasitumie maji ya chupa hivi inaingia akilini kweli hii!!!?? Ningependa kutumia nafasi hii kuwajulisha mashabiki zangu waliokutana na story hizo kuwa sio za kweli ni zenye lengo la kudhoofisha Mahusiano yetu mazuri ya wasanii Wa Africa mashariki..kama BigEye ya Uganda ilivyowahi kuandika habari za upotoshaji Kati yangu na Jose Chameleone.. Pia Nawasihi @Bongofive ni vyema mtambue Nafasi yenu kwenye jamii kwa sasa, Kuweni makini na baadhi ya habari mnazo post ama kureport kutoka baadhi ya mitandao, zinavunja mahusiano mazuri ya wasanii wa East Africa…kumbukeni kuna watu wana tabia ya kujudge kitu kwa kusoma kichwa cha habari tu pasipo kufuatilia undani wa habari…Yawezakuwa mwaandika kwa nia njema tu, lakini ni vyema muwe mnapata na uhakika kwanza kabla ya kuripoti, hususan story za kutengeneza chuki kama hizi….kufanya hivyo ndiyo mtasaidia kukuza industry yetu ya East Africa…
CloudsFM: UHUSIANO WA YOUNG KILLER NA MPENZI WAKE WATIMIZA MIAKA NANE
Ni mara chache sana kwa masupastaa kufunguka kuhusu mahusiano yao ya kimapenzi, ni wachache sana ambao wako tayari kuweka mambo wazi kama msanii Young Killer ambaye ameweka wazi uhusiano wake na mwanadada Halimaty.
Zitto:Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
Nimepokea taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujiuzulu na nimeshangazwa na sababu alizozitoa kujiuzulu…. http://t.co/ppUPR660ro
— Zitto Ruyagwa Kabwe (@zittokabwe) December 16, 2014
Tunatoa shukrani sana kwa wananchi wote ktk maeneo mbalimbali waliotuamini na kutuma ridhaa kuongoza mitaa/vijiji. #Uchaguzi2014 — MNYIKA John John (@jjmnyika) December 16, 2014
Kutokana na ushauri wa wananchi, wanachama na viongozi; Kamati Kuu itakuja na mapendekezo nini kifanyike hasa ktk ukiukwahi wa kanuni
— MNYIKA John John (@jjmnyika) December 16, 2014
Unyama wa kutisha kwa watoto, Mungu atawaadhibu waliotenda na kuwapumzisha kwa Amani Watoto hao. — Lameck Ditto (@Lameckditto) December 16, 2014
Prayers to my lovely mother she is sick,sick sick…….am feeling sick too,mungu nipe nguvu.
— T.I.D (@TIDofficialone) December 15, 2014
Njia nzuri ya ku-deal na mtu mpya kwenye Maisha ni KUTOMPANDISHA sana na KUTOMSHUSHA sana, Hata kama ni Star/Tajiri au Mwenzangu na mimi — Ben Pol (@IamBenPol) December 15, 2014
Matokeo uchaguzi Kilwa: Vijiji: 86 CCM-47 CUF-38 CHADEMA-1 VITONGOJI CCM-168 CUF-109 Vijiji vinne uchaguzi utarudiwa tena. — Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) December 16, 2014
Tafiti za awali katika maeneo yaliyoshiriki uchaguzi S/Mitaa zinaonyesha ongezeko kubwa la wananchi kupigia kura vyama vya upinzani. — Dr Wilbrod Slaa (@wilbrodslaa) December 16, 2014
Hatutapumzika mpaka pale nchi yetu itakapopata uongozi, dira & mtazamo mpya kufika kule Watanzania wanapotaka na wanapoamini inaweza kufika. — Dr Wilbrod Slaa (@wilbrodslaa) December 16, 2014
Bora mgombane wakati mnajenga halafu mpatane ujenzi ukikamilika kuliko mpendane wakati mnajenga halafu mgombane mkishakamilisha.-Swebe — MASANJA (@mkandamizaji) December 16, 2014
Breaking News:Basi la Kampuni ya Mohammed Trans limepata ajali eneo la Makomero,mpakani mwa Singida na Tabora na kuua watu sita. Chanzo:#ITV
— millardayo.com (@millardayo) December 16, 2014
Sawa inawezekana sababu ziko nje Ya uwezo wenu…!sasa Network inasumbua ndani Ya masaa 24 kweli!? Mnategemea watu waishije!? #Tanesco
— Elizabeth Michael (@OfficialLuluM) December 16, 2014