Kwenye 255 ya leo December 18 story zilizosikika ni pamoja na zawadi aliyoitoa Dr. Dre, wimbo mpya wa msanii Ray C na pia kuhusu taarifa zilizotoka kwenye msiba wa Aisha Madinda.
Rapper na mfanyabiashara Dr. Dre ametoa zawadi kibao pamoja na fungu la kama dola 10,000 kwa kila mtu ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ambayo inasimamia masuala yake ya Kisheria kama bonus kwa kazi yao nzuri 2014.
Msanii Ray C amesema ameahirisha kutoa wimbo wake mpya siku ya leo kutokana na kutokea kwa msiba wa aliyekuwa mnenguaji wa Twanga Pepeta, Aisha Madinda.
Ray C amesema anatarajia kuuachia wimbo huo ndani ya wiki ijayo japo kwa sasa tayari unapatikana kwenye mitandao.
Mazishi ya Aisha Madinda iliyokuwa yafanyike leo yameahirishwa kutokana na mwili wake kuendelea kufanyiwa uchunguzi Hospitali na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho baada ya uchunguzi huo kukamilika.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook