Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
CCM km Chama kinachotawala kinapaswa kujitenga na waovu, wabunge wake tunapaswa kuwa wakali dhidi ya uovu, tunapaswa kuongoza kwa uadilifu!
— Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) December 23, 2014
CCM ikishindwa kuongoza vita dhidi ya uovu, maadili ya Taifa yataporomoka. Taifa litaanguka. Hatuwezi kuwa tayari kuona CCM ikishindwa! — Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) December 23, 2014
Kuwageuza waovu wachache kuwa ndiyo CCM yote si sahihi. Kila mtu abebe msalaba wake. Tutazunguka nchi nzima kuilinda CCM kwa kusema ukweli!
— Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) December 23, 2014
Marcio Maximo aondoka rasmi nchini kurejea kwao nchini Brazil na ndege ya shirika la ndege la EMIRATES! http://t.co/v13roqsMIh — shaffih dauda (@shaffihdauda1) December 23, 2014
Tanzania ndio nchi ambayo msanii anaweza akawa hana hata kitanda lakini akakwambia amefanya video ya milioni 40.
— SONGA (@NiiteSonga) December 23, 2014
“Kama Rais alikuwa hajui anachokisema, basi nchi iko hatarini. Kama alijua, basi alikiuka katiba, na nchi iko hatarini zaidi” – Lissu
— Babu Sikare (@AlbinoFulani) December 23, 2014
Zitto Kabwe :Kuweka rekodi sawa, PAP ( sio IPTL ) wamelipwa tshs 306 bilioni. Alizosema Rais ni zile zilizokuwa Benki kama taslimu na dhamana za Serikali. Ambazo hakusema ni zile ambazo zililipwa na TANESCO baadaye. Ifahamike hadidu rejea ( Terms of References ) kwa CAG kufanya uchunguzi zilitolewa na PAC, hivyo PAC ndio yenye mamlaka ya kuzisemea, kuzielezea na kuzitolea ufafanuzi. Kwenye eneo hili Rais hakuwa sahihi na Ikulu inapasa kurekebisha. Jumla ya fedha ambayo PAP wamelipwa kutoka akaunti ya #TegetaEscrow Ni tshs 306 bilioni.
Blogs
Saleh Jembe
DIDA NDIYE MCHEZAJI WA KWANZA KUMKARIBISHA TENA PLUIJM YANGA
Kipa namba moja wa Yanga, Deo Munishi ‘Dida’ alikuwa mchezaji wa kwanza kumkaribisha Kocha hans van Der Pluijm siku aliyoanza mazoezi.
Pluijm amerejea Yanga baada ya aliyekuwa anainoa, Marcio Maximo, kutimuliwa.
Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Loyola, Dida alikwenda moja kwa moja na kumfungulia mlango Pluijm, akamkaribisha na baada ya hapo akaendelea na shughuli zake.
Michuzi:Katibu mkuu mpya wa Yanga atangaza mikakati yake ya kuhakikisha Klabu inajiendesha kiuchumi
Katibu mpya wa Yanga Dk. Jonas Tiboroha, ametangaza mikakati yake ya kuhakikisha Yanga inajiendesha kiuchumi ikiwa ni pamoja na kupitia upya mikataba yote ya wadhamini.
Akizungumza Makao Makuu ya Klabu hiyo leo, Tiboraha alisema kuwa Yanga ni klabu kubwa hiyo ni wakati wa kujiendesha yenyewe badala ya kutegemea mtu binafsi na kwamba haiwezi kuwa na mikataba ambayo haikithi maslahi ya klabu hiyo.
“Yanga ni bidhaa inayojiunza yenyewe uwezi kuingia mkataba wake sawa na Stand United, haiwezekani ikapata mgao sawa kama wanafunzi wa shule ya msingi unawapanga mstari unawambia haya kila mtu unamgawia pipi moja moja na wanaridhika, haiwezekani ni lazima Yanga iwe tofauti.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook