Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
….tank God ….mchongo ushaisha Kaa tayari kwa mkao wa kula…1/1/2o15.. damian_soul 2gether with..… http://t.co/0wmXpUs3im
— Damian Soul (@damiansoultz) December 23, 2014
#Blessings joh_makini pancholatino damian_soul..1/1/2015…stay tuned… http://t.co/kpcZkpbsMB — Damian Soul (@damiansoultz) December 23, 2014
Wakuu….wakati mkitafakari HOTUBA YA RAIS..kuhusu #Escrow Nawatakia x-mas njema !Nawapenda Sana!Mungu awabariki… pic.twitter.com/75ms3JoNOZ
— Halima James Mdee (@halimamdee) December 24, 2014
Mwaka huu Mashindano Ya ma Miss bahati imeangukia washindi wa pili,Miss universe No1 afya sio njema kwahyo No2 atawakilisha ktk mashindano — Elizabeth Michael (@OfficialLuluM) December 24, 2014
Leo tumepeleka misaada mbalimbali na kula keki na kituo cha watoto yatima cha “Mwandaliwa Orphanage Centre”… http://t.co/k24xO2jp9s
— ThePwaarific (@Cpwaa) December 24, 2014
Thank you so much Mr president @jmkikwete …. daima nitaendelea kujituma na kuhakikisha naitumikia vyema nchi yangu pic.twitter.com/I4RCRSmWB2 — Diamond Platnumz (@diamondplatnumz) December 23, 2014
Nawatakia wote heri ya Krimas. Amani na iwepo duniani.
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) December 24, 2014
Thanking God for the gift of life and family as we celebrate Christmas tonight. Because of Him, our cause is righteous. #PamojaDaima — Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) December 24, 2014
#EnziZile Hii ndo mida yangu ya kwenda kufuatilia nguo za sikukuu kwa fundi.. Halafu kila ukienda… http://t.co/OElrbUJtSa
— #BongoHiphop (@FidQ) December 24, 2014
Proin Wanawake Taifa Cup kuzinduliwa rasmi Januari Mosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza http://t.co/QudH4wlwHv — TFF TANZANIA (@Tanfootball) December 24, 2014
Proin Wanawake Taifa Cup kuzinduliwa rasmi Januari Mosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza http://t.co/QudH4wlwHv @jamalmalinzi
— TFF TANZANIA (@Tanfootball) December 24, 2014
Ligi Daraja la Pili (SDL) inayochezwa katika makundi manne tofauti inaingia raundi ya nne kesho http://t.co/ug98CS6K20 — TFF TANZANIA (@Tanfootball) December 24, 2014
Naomba nichukue hii fursa hii kukutakieni heri ya Noel na tumwombe Mungu atuvushe salama 2015,uwe mwaka wa mafanikio kwetu sote.
— Jamal Malinzi (@jamalmalinzi) December 24, 2014
Blog
Jamii Forums
Ajali iliyohusisha magari mawili imesababisha waliokuwa kwenye gari dogo kupoteza maisha maeneo ya Nzega, inaaemekana chanzo cha ajali ni speed ya gari dogo na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha.
Saleh Jembe
FIRST ELEVEN YA YANGA YAANZA KUJIPANGA HIVI
Baada ya kukamilisha siku nne akiwa kazini anainoa Yanga, Kocha Mholanzi, Hans van Der Pluijm tayari amepata kikosi cha kwanza atakachoanza nacho kuivaa Azam FC.
Timu hizo, zinatarajiwa kuvaana katika mechi ya Ligi Kuu Bara, itakayopigwa Desemba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.
Pluijm alianza kibarua cha kukinoa kikosi hicho Jumamosi ya wikiendi iliyopita mara baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mbrazili, Marcio Maximo kutimuliwa.
Katika mazoezi yake hayo ya siku nne, kocha huyo alionekana akikiandaa kikosi hicho kwa kuwapanga pamoja na kuwapa mbinu mbalimbali za ndani ya uwanja kuanzia mabeki, viungo na washambuliaji.
Kocha huyo, katika kikosi hicho cha kwanza kinatarajiwa kuwa na sura mpya nne zitakazoanza kuonekana kwenye mechi dhidi ya Azam FC, ambazo ni Salum Telela aliyekuwa anaanzia benchi, Danny Mrwanda, Amissi Tambwe na Akpah Sherman waliotua kuichezea timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo.
TAMBWE ANOGA YANGA, AOMBA APANGWE NA MLIBERIA WATU WAONE KAZI
Straika mpya wa Yanga Mrundi, Hamisi Tambwe, amemuangalia straika Mliberia, Akpah Sherman na kutamka kuwa atafurahi kama akianzishwa naye kwenye kikosi cha Yanga.
Mastraika hao wote, walijiunga na timu hiyo hivi karibuni kwenye dirisha dogo la usajili, Tambwe yeye amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Mliberia miaka miwili kwa ajili ya kuichezea Yanga inayojiandaa na Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Washambuliaji hao, tayari wameshaanza kufanya mazoezi pamoja ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuendelea kutimua vumbi Desemba 26, mwaka huu.
Tambwe alisema alimuona mshambuliaji huyo kwa mara kwanza kwenye mchezo wa Nani Mtani Jembe 2, yeye akiwa anaichezea Simba ambayo ilimalizika kwa Yanga kufungwa mabao 2-0 na kuukubali uwezo wake.
Tambwe alisema, mshambuliaji huyo ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao na msumbufu kwa mabeki wa timu pinzani, hivyo anaamini akicheza naye pamoja atafunga mabao mengi.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook