Msanii wa Hiphop kutoka kundi la Kikosi cha Mizinga, Kala Pina amesema siku ya mkesha wa Mwaka mpya ambayo ni kesho December 31 kutakuwa na show kubwa ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 ambayo itafanyika katika Viwanja vya Msasani Club ambapo amesema atasindikizwa na LWP, Country Boy, Big Dog Pose, Lufunyo na mastaa wengine wengi.
Pina amesema kuanzia mwakani kutakuwa na show kila Jumamosi kutakuwa Msasani Club na pia watakuwa wakiuza vitu mbalimbali ikiwemo T-shirt na vitu mbalimbali.
Msanii Wema Sepetu amesimulia namna Instagram ilivyomsaidia kukutana na muigizaji Van Vicker kutoka Ghana, mpaka namna walivyofanikisha kurekodi movie hiyo.
Wema amesema kuwa gharama za kutengeneza movie hiyo walichangia yeye na Vicker hivyo hata mapato watagawana pia, itazinduliwa March 2015 na kuzinduliwa nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Nigeria, Ghana na Uingereza.
Wadau wa Bongo Movie ikiwemo Bodi ya Filamu, Wizara pamoja na wasanii wamekutana leo kujadili juu ya mvutano uliopo kuhusu bei ambayo inapaswa kutumika kuuza kazi za movie za Tanzania baada ya Kampuni ya Steps kushusha bei mpaka sh. 1000/=.
Siku ya Jumamosi December 27 familia ya producer Swizz Beats na mwanamuziki Alicia Keys walifanikiwa kupata mtoto wao wa pili wa kiume, ambapo kuzaliwa kwa mtoto huyu kunafanya Swizz kuwa na jumla ya watoto watano mpaka sasa, watatu ni wa kike aliowapata kabla ya ndoa yake na Alicia.
Mwaka 2014 hauishi vizuri kwa DJ Mustard na YG ambapo kuna beef ya chinichini kati yao kupitia mtandao wa Instagram kwamba kutokana kudhurumiana hela kati yao, DJ Mustard alisema hajui kitu kuhusu YG kwa kuwa mpaka leo hajalipwa pesa zake anazomdai.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook