Baada ya kumshuhudia nahodha wake Steven Gerrard akiitoa salamu kwamba anaitumikia klabu hiyo katika msimu huu kama utakuwa msimu wake wa mwisho baada ya miaka 26 katika klabu hiyo wekundu wa Anfield wataongozwa na mchezaji mwingine .
Klabu ya Liverpool inajiandaa kumtangaza kiungo Jordan Henderson kuwa nahodha wake mpya baada ya kuondoka kwa Steven Gerard mwishoni mwa msimu huu.
Henderson alijiunga na Liverpool misimu mitatu iliyopita akitokea Sunderland na baada ya kuanza kwa kasi ya chini amekuja kuwa mchezaji muhimu kwenye klabu hiyo kiasi cha kuaminiwa na kuwa nahodha mpya.
Bado kocha wa Liverpool, Brendan Rogers hajaweka wazi uamuzi huu na inatarjiwa kuwa Jordan atatangazwa kushikilia nafasi hiyo muhimu baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Pamoja na kuwepo kwa taarifa kuhusu Henderson kukabidhiwa mikoba kama nahodha mpya, bado haijafahamika nani atakuwa nahodha msaidizi kwenye klabu hiyo na inaaminika kuwa huenda kiungo mshambuliaji Raheem Sterling akateuliwa kuwa nahodha msaidizi.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook