Mwaka wa 2014 ulikuwa mwaka mzuri kwa nyota wa muziki wa Pop, Taylor Swift baada ya mwanamuziki huyo kumaliza akiwa ameongoza kwenye orodha ya wasanii waliouza albamu nyingi nchini Marekani.
Kwa mujibu wa kampuni ya Nielsen Music, album ya 1989 iliyotolewa na Swift mwenye umri wa miaka 25, iliuza jumla ya nakala milioni 3.6 idadi ambayo ilikuwa kubwa kwa kopi za albamu zote kwa mwaka 2014.
Album ya the ‘Frozen’ ambayo nyimbo zake zilitumika kwenye movie ya ‘The Crown’ ilifuatia kwa mauzo ikiwa imeuza nakala milioni 3.53.
Cha ajabu ni kwamba album hii ya The Crown iliongoza kwa mauzo kwa kipindi cha miezi 12 kabla ya kupitwa kwenye mauzo kati wiki za mwisho za mwezi Desember ambapo ilipitwa na albamu ya Taylor Swift baada ya albamu hiyo ya 1989 kuuza kopi 326,000 katika kipindi cha wiki moja.
Album hizi mbili ndio album pekee zilizofanikiwa kuuza kopi milioni 3 kwa kipindi cha mwaka 2014, Sam Smith alishika nafasi ya tatu kwa kuuza album ya The Lonely Hour ambayo iliuza kopi milioni 1.21 ikifuatiwa na albamu za Beyonce, Lorde na One Direction pamoja na album ya mwanamuziki mkongwe Barbara Streisand.
Disney Music Group ambao walisimamia album ambazo zimetumika kama soundtrack kwenye movie za Frozen na Guardians of The Galaxy wamefanikiwa kuingiza albamu mbili kwenye album tano bora kwa mara ya kwanza kwenye historia ya takwimu za Nielsen Music.
Hii ni mara ya pili kwa Taylor Swift kumaliza mwaka akiwa na album bora kimauzo Marekani.
Chati Rasmi ya album za Marekani kwa Mwaka 2014
1.Taylor Swift – ‘1989’
2.Disney Music Group – ‘Frozen’ soundtrack
3.Sam Smith – ‘In the Lonely Hour’
4.Pentatonix – ‘That’s Christmas To Me’
5.Disney’s Hollywood Records – ‘Guardians of the Galaxy’ soundtrack
6.Beyoncé – ‘Beyoncé’
7.Barbra Streisand – ‘Partners’
8.Lorde – ‘Pure Heroine’
9.One Direction – ‘Four’
10.Eric Church – ‘The Outsiders’
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook