Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Ni vema kudumisha ujirani mwema Afrika Mashariki. Tunatatua mgogoro wa magari ya watalii Kenya na Tanzania kwa mafanikio ya wote.
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 6, 2015
TANGAZO: Sasa feat&collabo ni KUSAIDIANA na wala si muendelezo wa ule mfumo wa wasanii kushirikiana ili kuleta ladha tofauti au kupimana ✔ — #BongoHiphop (@FidQ) January 6, 2015
Nampongeza Prof. Tolly Mbwette kwa kuzindua maktaba yake kwa matumizi ya umma, Mbwette Professorial Library iliyopo Kimara Mavurunza.
— MNYIKA John John (@jjmnyika) January 6, 2015
EWURA imepunguza bei za mafuta nchini baada ya kudorora kwa uchumi Ulaya. Petroli itauzwa sh.1955, dizeli sh.1846, mafuta ya taa sh.1833/ltr — Jamii Forums (@JamiiForums) January 6, 2015
Utumwa sio mbaya kama ukiwa mtumwa wa kupenda ubinadamu
— Nick Mweusi (@nikkwapili) January 6, 2015
CloudsFM: MAN WATER ANAAMINI “MWANA” YA ALLY KIBA IMLETEE TUZO MWAKA HUU
Producer Man Water wa combination sound amefunguka kuwa kutokana na kufanya vizuri kwa ngoma alizoachia mwaka 2014 basi anategemea vitu vikubwa mwaka huu ikiwemo tuzo na deal nyingi za kurecord mwaka huu…
Blogs
Mwananchi:
Baadhi ya wanawake wa Kitanzania waliofungwa katika magereza ya China na Hong Kong, walishika ujauzito kama moja ya mbinu ya kupitisha dawa za kulevya bila kugundulika kwenye viwanja vya ndege na mipaka mingine ya kimataifa. Mwananchi limebaini.
Watanzania wanne walio katika magereza ya China na Hong Kong walijifungua watoto kwa nyakati tofauti wakiwa wanatumikia vifungo na wamekiri kuwa walibeba ujauzito kama mbinu ya kupitisha dawa hizo bila kukaguliwa.
Watoto wanaozaliwa magereza baada ya kufikisha mwaka mmoja hupelekwa katika vituo vya watoto yatima na kusomeshwa na Serikali ya China hadi pale wazazi wao watakapomaliza adhabu.
Saleh Jembe: STRAIKA ALIYETIMULIWA DAR NA MAXIMO APATA TIMU HISPANIA
Unamkumbuka yule straika aliyebatizwa jina la “bonge”, alikwenda kufanya mazoezi Yanga, Kocha Marcio Maximo akamtosa, sasa yuko Hispania.
Suleiman Abdallah Mbarouk amesema anaendelea vizuri katika klabu yake ya daraja la pili ua Jerez ambayo imempeleka kwa mkopo Fosehill.
“Huku naendelea vizuri kabisa, sasa nimerudi Uingereza kwa muda kwa ajili ya mapumziko ya mwanzo wa msimu.
“Kitu ambacho ninaweza kusema ni masikitiko yangu kuhusiana na yule aliyekuwa kocha wa Yanga, (Marcio) Maximo. Alinifanyia kitu kibaya kwa kushindwa kunipa nafasi hata kidogo kuonyesha uwezo wangu.
“Nilikuja Yanga kufanya majaribio, lakini hakunipa nafasi hata kidogo. Badala yake alionyesha hofu kama ningefanikiwa basi ningeweza kuwanyima nafasi ndugu zake Wabrazil.
“Wanasema mimi bonge, vipi nacheza Hispania, nacheza England? Kwani soka la England na kwetu Afrika lipi lipo juu,” alisema.
“Nasikia kafukuzwa, ila alinionea sana. Sasa nacheza kwenye timu yangu, nimecheza mechi tisa, nimefunga mabao saba. Nitarudi Spain Januari 9 ili kuendelea na kazi.”
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook