Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Kwa namna moja au nyingine “WAHENGA” walichangia kupotosha jamii za kale na za sasa pia. #Usiafiki_Kila_Walichosema
— Kusingekuwa_Na_Muzik (@NikkiZohan) January 9, 2015
Tuhimize mijadala ya maendeleo. Tusitumie nguvu nyingi kujididimiza kwa mijadala ya uzushi, fitna na chuki.Msiyumbishwe na wanasiasa. — Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 9, 2015
Kesho nazungumza na wenye magari ya kitalii mjini Arusha waliozuiwa kuingia uwanja wa ndege wa Nairobi katika siku za hivi karibuni
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 9, 2015
Ntakuwa viwanja vya Riverside Shuttles saa 2asubuhi kuongea na wamiliki wa magari yaendayo Kenya kusikiliza kero wanazozipata Jomo Kenyatta — Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 9, 2015
Facebook
Nay wa Mitego: Hawa wanaosanda gemu, watuachie muziki wetu. au yawezakua kick ikuboost kwa wasiokujua kama ulikua unafanya music.
#kilimoUti #waMgongo
Kabwe: LINDI YAWEZA KUWA SRI LANKA YA TANZANIA
( niliandika makala haya mwaka 2012 )
WATANZANIA wengi tukisikia jina Sri Lanka jambo kubwa linalotujia kwa haraka ni ama chai au Vita ya Tamil Tigers. Nakumbuka tulipokuwa darasa la sita Shule ya Msingi tulisoma ‘Chai Sri Lanka’ na kusoma miji kama Kolombo, Batikaloa na Trinkomalee (Colombo, Batticaloa, Trincomalee). Lakini tulipashwa sana habari kuhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka takribani 30. Juzi nilikuwa Sri Lanka. Vita imekwisha mwaka 2009. Chai ipo nyingi sana. Mwaka 2010, Sri Lanka iliuza nje jumla ya tani 314,000 za chai yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.37 na hivyo kuongoza duniani kimapato ingawa Kenya ilisafirisha chai nyingi zaidi, tani 441,000.
Hata hivyo, kutokana na ubora wa zao hilo kuwa chini kidogo Kenya ilipata dola za Marekani milioni 800 tu. Mwaka huo Tanzania, yenye eneo kubwa zaidi la kulima kuliko nchi zote hizo, iliuza nje tani 34,000 tu na kupata dola za Marekani milioni 61 hivi. Licha ya kwamba Tanzania ni nchi ya nne kwa kuzalisha chai Afrika baada ya Malawi, Uganda na Kenya, bado inaweza kuwa katika nafasi ya juu duniani iwapo tukiamua kuwa makini katika mambo tunayofanya na kupenda kufanya mambo makubwa.
Siku hizi napenda kujua historia za nchi katika kupambana na umasikini wa watu wao. Lengo ni kuelewa juhudi za nchi mbalimbali katika kuleta maendeleo ya watu na kujifunza pale ambapo nchi zimefanikiwa. Ukitembea mitaa ya Jiji la Colombo unaona mji mzuri msafi uliopangwa vema na kila mtu anaonekana kushughulika. Njia nzuri ya kujua ukweli wa maisha ya watu ni kuzungumza nao.
Mara nyingi hutumia madereva wa teksi au bajaji kwa jiji kama la Colombo. Katika mazungumzo na baadhi ya madereva wa bajaji nilizokuwa natumia pale Colombo niliona mwelekeo mmoja, kwamba katika kipindi cha miaka 10 iliyopita maisha yao yamebadilika sana. Wakisifia kuisha kwa vita dhidi ya Tamil Tigers na kuongezeka kwa mapato yao kwa watu kutumia zaidi usafiri. Dereva wa bajaji wa Jiji la Colombo anaingiza wastani wa rupia 4000 (shilingi 45,000) kwa siku. Nilitaka kujua nini chanzo cha mabadiliko haya ya kipato ambacho hadi wenye bajaji wanafaidika nayo. Takwimu zao zinaeleza mengi sana. Serikali iliamua kupambana na umasikini na hasa umasikini wa vijijini.
Mwaka 2002 asilimia 22.7 ya wananchi wote wa Sri Lanka walikuwa wanaishi chini ya mstari wa umasikini. Ilipofika mwaka 2011, kiwango cha umasikini kilikuwa asilimia sita tu. Umasikini ulishuka kwa kiwango kikubwa katika maeneo ya vijijini. Katika kipindi cha miaka mitatu kati ya mwaka 2007 mpaka 2010 umasikini wa wananchi wa Sri Lanka walio kwenye sekta ya chai (estate sector) ulishuka kutoka asilimia 32 ya waliokuwa wanaishi chini ya mstari wa umasikini mpaka asilimia 11.4 na wale wa vijijini nje ya sekta ya chai umasikini ulishuka kutoka asilimia 24.7 mpaka asilimia 9.4 katika kipindi hicho. Nilipouliza zaidi kwa wanasiasa na viongozi wa serikali nikaambiwa kuwa mabadiliko makubwa yaliyotokea miaka ya karibuni yalitokana na serikali kufanya uamuzi mahususi wa kuelekeza fedha nyingi zilizokuwa zinakwenda vitani kwenye uwekezaji vijijini. Wanasema walitumia fedha nyingi kwenye ruzuku ya mbolea kwa wakulima, kusambaza umeme vijijini na kujenga barabara za vijijini. Siku niliyofika niliona kwenye moja ya magazeti yao ya kila siku, rais wao akizindua mtambo wa kuzalisha umeme katika Mji wa Trincomalee uliopo mashariki mwa nchi hiyo.
Nikajiuliza mbona na sisi tunatekeleza MKUKUTA na tunasema kwamba tunawekeza fedha nyingi sana vijijini? Mbona na sisi tunatoa ruzuku ya mbolea yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 60 kwa mwaka? Inakuwaje wenzetu wafanikiwe sisi tusifanikiwe? Tanzania imeanza kutoa mbolea ya ruzuku katika msimu wa mwaka 2006/2007 kama ilivyo kwa Sri Lanka. Wenzetu katika miaka mitatu, kiwango cha umasikini kimepungua kwa asilimia 15 kwa wananchi walio katika sekta hiyo ya kilimo na wanaoishi vijijini. Sisi katika kipindi cha muongo mmoja, 2001 mpaka 2011, umasikini umepungua kwa asilimia mbili tu. Moja ya sababu ya sisi kushindwa ni kwamba mfumo wa mbolea ya ruzuku umegubikwa na ufisadi wa hali ya juu sana. Mfumo huu umedhihirisha namna ambavyo kazi ya kupambana na ufisadi ni ya kimfumo zaidi maana kwa namna viongozi wa vijiji wanavyoiba mbolea ya ruzuku, unaweza kiurahisi kabisa kusema rushwa ni sehemu ya utamaduni wa Mtanzania. Siamini hivyo. Ninaamini kwamba mfumo wetu unazalisha wala rushwa, walafi na watawala wenye tamaa na wasiotosheka kama nilivyoeleza katika makala zangu zilizotangulia. Je, tukiondoa ufisadi wa mbolea ya ruzuku tunaweza kupata mafanikio ambayo wenzetu wameyapata? Sina jibu wala jawabu la swali hili. Hata hivyo, ninaamini kwamba kutofanikiwa kwetu ni zaidi ya ufisadi. Ni kutofanya kazi kwa bidii? Ni kukosa umakini? Ni kutofurahia mafanikio? Ni kukosa uongozi thabiti unaoweza kusimamia mchakato wa maendeleo kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Taifa?
Hebu tutazame pamoja takwimu hizi. Sri Lanka ina ukubwa wa kilometa za mraba 65,000. Mkoa wa Lindi una ukubwa wa kilometa za mraba 66,000. Sri Lanka ina Pato la Taifa la Dola za Marekani bilioni 60 mwaka 2011, Tanzania Pato lake la Taifa ni dola za Marekani bilioni 24. Sri Lanka ina jumla ya watu milioni 20, Tanzania ina jumla ya watu milioni 45, Mkoa wa Lindi una jumla ya watu 750,000 hivi. Sri Lanka na Tanzania zote zina bajeti ya dola za Marekani bilioni tisa hivi. Uchumi wa Sri Lanka unategemea sana zao la chai na utalii kwa fedha za kigeni. Mkoa wa Lindi una eneo kubwa zaidi la Kilimo kuliko Sri Lanka nzima hasa ukizingatia katika hekta milioni 5.2 zinazofaa kwa kilimo ni hekta 500,000 tu ndio zinalimwa. Zao la korosho laweza kuwa chai ya Lindi. Kilometa za mraba 18,000 za Mkoa wa Lindi ni Selous Game Reserve, Kilwa ni kivutio kikubwa cha utalii wa kila namna na Mkoa wa Lindi una fukwe ambazo hazijawahi kuguswa tangu dunia iundwe na Mola.
Sri Lanka hawana gesi asilia. Lindi na hasa Wilaya ya Kilwa ndio mzalishaji mkubwa wa gesi asilia hapa nchini. Pia sehemu kubwa ya gesi iliyogunduliwa hapa nchini ipo katika Mkoa wa Lindi ingawa wengi wetu hudhani kwamba ipo Mkoa wa Mtwara. Lakini Lindi na Mtwara sawa tu. Mtwara ina kilometa za mraba 16,000 (chini ya eneo la Lindi lililopo Selous). Tufanye Lindi na Mtwara kwa pamoja ndiyo Sri Lanka ya Tanzania. Tunaweza kujenga uchumi wa dola za Marekani bilioni 60 kwa Lindi na Mtwara? Tunaweza kufanya mikoa hii iwe na kiwango cha umasikini chini ya asilimia tatu ya wananchi wake? Tunaweza kuingiza watalii 800,000 kwa mwaka kwa mikoa hii tu? Tunaweza kuuza nje korosho yenye thamani ya dola za Marekani angalau milioni 600? Tunaweza kutumia sehemu ya mapato yatokanayo na gesi asili kujenga miundombinu ya barabara, umeme, reli na maji kwenye wilaya zote za hii Sri Lanka yetu? Tunaweza kuwekeza kwenye elimu kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora? Tunaweza kuhakikisha kuwa asilimia 97 ya wakazi hii Sri Lanka yetu wanapata huduma za afya?
Majibu ya maswali yote haya ni NDIO. Utashi. Utayari. Uthubutu. Hebu tuthubutu kuiweka Sri Lanka Tanzania. Lindi na Mtwara ni zaidi ya Sri Lanka. Nikipata fursa ya kuandika tena nitaandika kuhusu uwekezaji kwenye elimu nchini Sri Lanka na kwamba haki ya kupata elimu mpaka Chuo Kikuu ni haki ya kikatiba yenye kuweza kudaiwa mahakamani.
CloudsFM: TAHARUKI UFARANSA
Huku maafisa wa polisi wakiwazingira washukiwa wawili wa ugaidi , kuna taarifa mpya kwamba Mwanamume tofauti aliyejihami kwa bunduki, amewateka nyara watu ndani ya duka mjini Paris
Washukiwa wanaozingirwa ni wale waliowaua watu 12 waliokuwa wakifanya kazi na jarida la vibonzo la Charlie Hebdo.
Taarifa za mwanamume huyu mwingine kuwateka nyara watu 5 ndio zimejiri sasa hivi.,
Idadi kubwa ya polisi iliingia katika eneo la Porte de Vincennes Mashariki mwa Paris,baada ya mwanamume huyo kuripotiwa kufyatua risasi huku akiwateka nyara watu wnegine 5.
Inaarifiwa mshukiwa huyu ni yule aliyemuua polisi mwanamke mjini humo Alhamisi.
Washukiwa wa shambulizi la Charlie Hebdo pia wamewashika mateka watu kadhaa ambao idadi yao haijajulikana.
Washukiwa hao wanaarifiwa kujificha ndani ya kituo cha kupiga chapa na inasemekana wamesema kuwa wako tayari kufa.
Blog
BBC: Huku maafisa wa polisi wakiwazingira washukiwa wawili wa ugaidi , kuna taarifa mpya kwamba Mwanamume tofauti aliyejihami kwa bunduki, amewateka nyara watu ndani ya duka mjini Paris
Washukiwa wanaozingirwa ni wale waliowaua watu 12 waliokuwa wakifanya kazi na jarida la vibonzo la Charlie Hebdo.
Taarifa za mwanamume huyu mwingine kuwateka nyara watu 5 ndio zimejiri sasa hivi.,
Idadi kubwa ya polisi iliingia katika eneo la Porte de Vincennes Mashariki mwa Paris,baada ya mwanamume huyo kuripotiwa kufyatua risasi huku akiwateka nyara watu wnegine 5.
Inaarifiwa mshukiwa huyu ni yule aliyemuua polisi mwanamke mjini humo Alhamisi.
Washukiwa wa shambulizi la Charlie Hebdo pia wamewashika mateka watu kadhaa ambao idadi yao haijajulikana.
Washukiwa hao wanaarifiwa kujificha ndani ya kituo cha kupiga chapa na inasemekana wamesema kuwa wako tayari kufa.
Watu Twelve walipigwa risasi na kufariki huku wengine 11 wakijeruhiwa,katika shambulizi la kwanza dhidi ya ofisi za jarida la Charlie Hebdo, jarida ambalo huchapisha vibonzona lenye uhuru wa hata kukejeli dini ya watu.
Shambulizi hilo limewashangaza watu nchini Ufaransa na kote duniani.
Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa katika eneo la Dammartin-en-Goele yapata kilomita 35 kutoka Paris,lakini maafisa wamekana ripoti ya mauaji yoyote.
Mpango huo unajiri karibia masaa 48 baada ya shambulizi hilo katika afisi za gazeti hilo ambapo watu 12 waliuawa kwa kupigwa risasi.
Washukiwa hao wanaodaiwa kujihami vilivyo baadaye waliutoroka mji wa Paris wakitumia gari.
Saleh Jembe
OKWI AIFUNGULIA KESI YANGA, AIDAI SH MILIONI 107
SIKU moja baada ya uongozi wa Simba kutangaza kuachana na kipa Juma Kaseja, sasa unalazimika kupambana na kesi mpya dhidi ya kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Kupitia mwanasheria wake, Kampuni ya Agaba Muhairwe & Co Advocates ya Kampala, Uganda. Okwi amefungua kesi akitaka Yanga imlipe kitita cha jumla ya dola 62,000 (zaidi ya Sh milioni 107).
Mgawanyo wa madai hayo umegawanywa mara mbili, ukianza na dola 50,000 ambazo Okwi anaidai Yanga aliposajili ikiwa alilipwa nusu yake.
Pili, mshahara wake, dola 12,000 ambao pia hakulipwa na Yanga. Jumla inakuwa dola 52,000.
Tayari Agaba Muhairwe & Co Advocates wamewasilisha barua yenye kumbukumbu namba AM/129/ea kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Haki za Wachezaji.
Barua hiyo ya Januari 7, kopi mbili, moja imewasilishwa kwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na nyingine kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Mwanasheria huyo wa Okwi amesisitiza kwamba hawatafungua kesi yoyote kwa kuwa wanatoa hadi Februari 15 kuwa wameishalipwa fedha hizo.
Sehemu ya barua hiyo inaonyesha barua ya juzi inakumbushia barua nyingine kama hiyo ambayo kampuni hiyo ya mwanasheria iliitoa na kutaka Okwi awe amelipwa hadi Desemba 15, mwaka jana lakini haikufanyika.
Maana yake, iwapo Yanga watashindwa kufanya hivyo watakuwa tayari kufungua kesi ya madai kuhakikisha wanapata fedha zao na haina ubishi watakwenda Fifa ambayo wameisha itaarifu kuhusiana na deni hilo.
Okwi aliondoka Yanga baada ya uongozi kumtema katika hatua za mwisho za usajili wa dirisha dogo na Simba ikamsajili, hali iliyozua tafrani kubwa. Baadaye TFF ilimpitisha Okwi kuichezea Simba na Yanga haikuwa imekubaliana na uamuzi huo.
Kopunovic: Waleteni hao Yanga
Na Sweetbert Lukonge, Zanzibar
BAADA ya kikosi cha Simba kufanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kishindo, kocha mkuu wa timu hiyo raia wa Serbia, Goran Kopunovic, ametamka wazi: “Waleteni hao Yanga.”
Jumatano iliyopita, kocha huyo aliyejiunga na Simba hivi karibuni akichukua mikoba ya Mzambia, Patrick Phiri, alikuwa ni mwenye furaha kubwa baada ya kuishuhudia timu yake ikipata ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Taifa Jang’ombe.
Matokeo hayo yamempa jeuri ya kutamka hivyo kwa kusema kuwa yupo tayari kupambana na timu yoyote ikiwemo Yanga ambayo imeonekana kufanya vizuri pia.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kopunovic alisema kuishuhudia timu yake ilipocheza na Mtibwa Sugar yeye akiwa jukwaani, aligundua mambo mengi ya kiufundi yaliyokuwa na upungufu.
“Vijana wanajitahidi sana kuzingatia maagizo yangu, jambo ambalo linanipa matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano haya.
“Kuna mabadiliko makubwa tofauti na nilivyowakuta, hivi sasa wanaweza kupambana na timu yoyote ile kwenye mashindano haya na kuibuka na ushindi, hata hiyo Yanga wataifunga kama tukikutana nayo,” alisema Kopunovic.