Muimbaji wa Msambinugwa Khalid Mohamed aka Tunda man amesema anatarajia kufungua bendi yake ya muziki hivi karibuni baada ya kukamilisha mipango yake.
Akizungumza na millardayo.com alisema; “Nimegundua kuwa muziki wa bendi ni muziki fulani ambao unaweza uka enjoy sana kwenye kuimba au una kwenye show unaweza uka enjoy tu sehemu yoyote unaofanya muziki mwanzo nilikuwa naona jamaa wakiimba na bendi wanapata tabu lakini tangu nianze kuimba muziki wa bendi nimegundua napata vitu vizuri kabisa kwa hiyo nafikiri ikishafika mwezi wa sita kila kitu kitakuwa tayari kwasabab nimeongea na The big boss chief Kiumbe kuhusiana na vyombo kanimbia basi sawa tutaanza kununua vitu taratibu kuanzia Guitar, Drums, Keybord kwa hiyo malengo yangu ishafika mwezi wa sita kwenda mbele show zangu niwe na bendi niwe na cabinaty yangu niwe na watu wa kupiga show yangu yoyote nitakuwa na bendi sitaki kupiga sijui kila Ijumaa au kila Jumamosi sehemu lakini kila show yangu lazima uwe unanibeba mimi pamoja na bendi yangu kwasababu nimegundua muziki wa bendi ni muziki mzuri mtu ana enjoy sana” — Tunda Man.
Hapa kuna sauti ya Tunda akiongea na millardayo.com, isikilize kwa kubonyeza play hapa.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook