Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Maisha huchanua na kusinyaa kutokana na ujasiri wako mwenyewe! Kua Jasiri!
— Izzo_bizness (@Izzo_bizness) January 21, 2015
Kila la kheri mdogo wangu Mbwana Samatta katika majaribio unayoyafanya huko Urusi kwenye klabu ya CSKA Moscow – milango ikufungulikie. — shaffih dauda (@shaffihdauda1) January 21, 2015
Tutaraji kumwona Samatta Champions league hivi karibuni? Mungu atamjaalia. Dua zetu zote kwake. Asante Shaffih K Dauda kwa picha
— Zitto Ruyagwa Kabwe (@zittokabwe) January 21, 2015
Facebook:
Mwananchi:Majambazi yateka kituo cha polisi, yaua askari wawili, yapora bunduki tano Rufiji:WATU 15 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za kivita na mabomu ya kurushwa kwa mkono wamevamia kituo cha polisi Ikwiriri wilayani Rufiji Mkoani Pwani na kuua askari polisi wawili na kupora silaha tano za SMG na mbili za kufyatulia mabomu ya machozi zilizokuwepo kituo hapo na kutokomea kusikojulikana. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa majambazi hao wamefanikiwa kuchukua silaha tano za moto na mbili za mabomu ya machozi zilizokuwepo kituoni hapo.
Blog
BBC: Mwanajeshi wa UK hatiani kwa kumbaka mtoto
Mwanajeshi mwingereza ameshtakiwa kwa kosa la kumbaka na kumdhalilisha mtoto mwenye umri wa miaka 6 nchini Austria.
Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mwanajeshi huyo ambaye hajatajwa alikamatwa mwezi Novemba katika eneo la Tyrol ambako alikuwa anafanya mazoezi yake ya kijeshi.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 10 mwezi Machi.
Msemaji wa kiongozi wa mashtaka alisema kua wendeshja mashtaka wanaamini kwamba mwanajeshi huyo aliingia nyumbani kwa familia ya msichana huyo akiwa mlevi nyakati za asubuhi na kufanya kitendo hicho.
Mwanajeshi huyo alipatikana katika chumba cha mtoto huyo baada ya babake kusikia kelele.
Alikamatwa mjini Neustift na ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miaka 10.
Msemaji wa kiongozi wa mashtaka aliambia BBC kuwa mtoto huyo alihojiwa na kiongozi wa mashitaka.
BBC: Arsenal yamsajili Krystian Bielik
Arsenal imekamilisha usajili wa kiungo wa kati Krystian Bielik mwenye umri wa miaka 17 kutoka kilabu ya Legia warsaw kwa kitita kisichojulikana.
Bielik aliichezea timu kubwa ya kilabu hiyo ya Poland mnamo mwezi Agosti akiwa na umri wa miaka 16.
Pia alishiriki katika mechi tano ya kilabu hiyo na mara moja katika ligi ya yuropa.Mchezaji huyo anayesifiwa na wengi anaweza kucheza katika safu ya kati na ile ya Ulinzi.
Mwananchi: Hospitali ya Mbeya yateuliwa kupima ebola
Mbeya. Hospitali ya Rufaa Mbeya (MRH), imeteuliwa rasmi kuwa na maabara maalumu ya kuwapima watu watakaohisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa ebola.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Mpoki Ulisubisya alisema hayo jana jioni alipozungumza mambo mbalimbali kuhusu changamoto zinazoikabili hospitali yake.
“Ni kweli Serikali imeiteua maabara yetu ya hospitali kuwa maabara maalumu ya kupima virusi vya ebola nchini na kwa sasa maandalizi yote yanakamilishwa na tutaanza kazi mwishoni mwa mwezi huu au mapema Februari’’ alisema.
Kwa kipindi cha miaka mitano sasa, Maabara ya Hospitali ya Rufaa Mbeya ni maabara ambayo imethibitishwa kimataifa kwa ubora na kwamba vipimo vikitolewa kwenye maabara hiyo vinakubalika hata nchi za Marekani na Uingereza.
Akizungumzia uboreshaji wa utendaji kazi amesema wafanyakazi kupitia kwa viongozi wao kwa sasa wameimarisha utendaji kazi.
Kuhusu chumba cha kuhifadhi maiti kwenye Hospitali hiyo, Ulisubisya amesema Serikali imempata mtu atakayejenga jengo kubwa la kuhifadhi maiti na kuliboresha ili kuendeshwa kwa ubia katika hali ya usafi na kisasa zaidi.
‘’Bila shaka unakumbuka , mfanyakazi wa chumba cha maiti aliwahi kumweleza Waziri kwamba ukifariki dunia ukiwa Mbeya maiti yako italazwa chini. Sasa Serikali imeamua kuchukua hatua ili kuboresha nyumba hizo ingawa wahusika watatakiwa kutoa mchango kidogo’’alisema.
TZA Millardayo.com: Daladala ziligoma leo Arusha, ni Bodaboda tu barabarani…
Waendesha bodaboda wa Arusha leo wamejikuta kwenye jukumu la daladala kusafirisha abiria baada ya mgomo wa daladala uliofanywa leo maeneo ya mji huo sababu ikitajwa ni kuanzishwa kwa route mpya wanayotakiwa kuanza hivi sasa kutoka Njiro na Moshono kuelekea mjini.
Wakazi wengi wa mji huo leo wamelazimika kutembea kwa miguu huku wengine wenye uwezo wakitumia usafiri wa bodaboda.
Ripota wa Blog ya Michuzi ambaye ameripoti kuhusu story hii amesema yeye pia alikuwa mmoja ya walioathirika kutokana na mgomo huo
Saleh Jembe
YANGA WAENDELEA KUISIKILIZIA TFF SUALA LA TAMBWE…
Uongozi wa Klabu ya Yanga umefunguka kuwa unasubiria kuona Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), litachukua hatua gani kutokana na kitendo cha mshambuliaji wake Amissi Tambwe kukabwa koo na mchezaji wa Ruvu Shooting.
Tambwe alichezewa rafu kadhaa na beki wa timu hiyo, George Michael, mpaka akachanika mdomoni lakini mwamuzi hakuchukua hatua yoyote.
Katika mchezo wa Jumamosi kati ya Yanga na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, kulikuwa na vurugu kiasi cha kufikia hatua mechi kusimama mara kwa mara.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, amefunguka kuwa wamesikitishwa na kitendo kilichotokea katika mchezo huo na kudai kuwa kuna matukio mengi ambayo hayakuwa sawa, hivyo wanawasubiri TFF kuona watachukua hatua gani kuhusiana na suala hilo.
“Hatukutaka kulizungumzia suala hili kwa watu na tulihitaji Watanzania waone wenyewe kama picha ilivyojieleza kwenye magazeti (anamaanisha Championi).
“Tunasubiri watu wenye dhamana ya mpira tuone watatoa maamuzi gani kuhusiana na mechi hiyo, kwani matukio mengi ambayo siyo mazuri yalijitokeza katika mchezo ule.
“Nadhani waamuzi wataandika ripoti yao, kamisaa wa mchezo pia ataandika na kila mmoja ameona, hivyo tunasubiri maamuzi yatakuwaje kwani kitendo kilichofanywa siyo kizuri na iwapo hakuna hatua watakayochukua tutajua cha kufanya,” alisema Tiboroha.
Alimalizia kwa kusema lengo ni kuhakikisha wachezaji wao wanakuwa na usalama kwa kutopatwa na matatizo.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook